Skip to main content

Posts

Showing posts from July 5, 2015

BREAKING NEWZZZ....HUYU JAMAA AKAMATWA NA MABILIONI YA PESA KWENYE BEGI MJINI DODOMA MDA HUU ...NI HATARIII

HUYU JAMAA MWENYE ASILI YA KIHINDI ANASWA NA HIZI PESA HAIJAFAHAMIKA BADO NI KWA AJILI YA KUFANYIA NINI...ENDELEA KUFWATILIA HAPA UPATE HABARI ZOTE

Kikosi cha Azam FC kimethibitisha kuwapokea hawa watatu toka nje ya TZ..

Golikipa  Nelson Lukong Bongaman , jamaa anatokea Congo ila ni Raia wa Cameroon. Ligi Kuu TZ bara inatarajiwa kuanza August 2015, Vikosi ya Timu za soka vimeendelea kujipanga na kuimarisha Vikosi vyao ili mambo yaende sawa msimu huu watoke na ushindi,  Azam FC  wamethibitisha kwamba safari hawako tayari kuukosa pia. Azam FC  jana ilithibitisha kuanza kuwapokea  wachezaji wa kigeni wanaotarajia kujiunga nao na kufanya majaribio na klabu hiyo, kwenye taarifa ya Klabu hiyo imeonesha jana usiku walitarajia kumpokea golikipa ambaye ni raia wa Cameroon,  Nelson Lukong Bongaman   ambaye alikuwa anachezea timu za Congo DRC. Jean Mugiraneza Babtiste Klabu hiyo ilitarajia pia kumpokea staa mwingine mida ya saa 2 asubuhi ambae ni raia wa Uingereza,  Ryan Burge . Nyota mwingine waliyemtaja kuwa watampokea ni mchezaji kutoka  Klabu ya APR  ya Rwanda,  Jean Mugiraneza Babtiste . Kikosi cha  Azam FC  kimeelekea Tanga kwa ajili ya maandalizi ya kukipiga na Klabu ya African Sport  kw

Black Ryno na albamu mpya, Nay Feat.Diamond imebuma? na Producer DX anamkubali nani?.

Black Ryno  amesema baada ya kumaliza masters yake  MZUMBE   sasa akili yake imekua na ataachia albamu yake muda si mrefu kwani sasa anajua nini anafanya ili kazi zake ziweze kuuzika na kumpatia faida zaidi…jamaa pia kasema atakua anauza kazi zake kupitia mitandao ya kijamii na kwenye  Supermarkets  kubwa ili zimfikie kila mmoja tofauti na zamani. Black Ryno Kingine kilichosikika leo kwenye 255 ni kumhusu  Nay wa Mitego  ambaye amefunguka na kusema hakuwa amepanga kutoa single yake ya  ‘Sina muda’  bali mashabiki ndio waliomlazimisha kwa sababu bado ‘ Mapenzi au Pesa’  ilikua ikifanya vizuri. Nay wa Mitego Amesema video zote zitatoka wakati wowote kuanza sasa. DX  kutoka  Noise Maker  kutoka Arusha amesema anamuelewa sana mtayarishaji chipukizi  Mesen Selector  kutokana na uwezo wake mkubwa..amekua akitayarisha nyimbo wakati huo huo ni mwanamuziki….ana ubunifu mkubwa kwenye kazi yake kwa sababu yuko sehemu tofautitofauti

Kumbe Kuna ugomvi kati ya Luteni Kalama na Inpector Haroun? sikilioza #Uheard (Audio)

Jana kupitia akaunti yake ya  @Instagram   mke wa  Luten Kalama  ametoboa mambo mengi kuhusiana na kundi la  Gangwe Mob   ambalo kwa sasa lina mgogoro mzito. Luteni Kalama mwenyewe amesema anashangaa kusikia  Inspekta Haroun   anasambaza maneno kwa watu kuwa yeye anazuiwa kufanya kazi na mke wake…ametoboa kuwa hata akipewa ela ya shoo anaenda mwenyewe na anampa ela ndogo tofauti na makubaliano yao..anasema ugomvi wao umedumu kwa  takribani miaka nane. Mke wake amesema aliwahi kwenda  Dar Live  akapigwa na mashabiki wakidai yeye ndio anaua kundi la Gangwe Mob kitu kinachotishia maisha yake..

Hii ndio klabu iliyomchukua Ramadhani Singano (Messi)

. Ikiwa imepita siku moja toka  Kamati ya Haki na Hadhi za Wachezaji ya TFF kuvunja mkataba wamchezaji Ramadhani Singano (Messi)  na iliyokuwa klabu yake Simba leo hii amesaini mkataba wa kuichezea klabu ya Azam Fc . Singano amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo inayonolewa na muingereza Stewart Hall na ataungana na kikosi hicho muda wowote kutokea hivi sasa. . Ikumbukwe kuwa wiki kadhaa zilizopita kulikuwa na utata wa ki mkataba kati ya Singano na Simba kwa zile tofauti zilizotokea ndani ya mkataba ambazo nakala ya mkataba wa mchezaji inaonyesha kumalizika mwezi june 2015 wakati ule wa klabu ukionesha june 2016. Chanzo: Saleh Jembe blog

Haya ndiyo Magari 10 ya gharama ya mastaa wa soka Ulaya 2015…

Moja ya starehe za mastaa wengi wa soka duniani ni pamoja na kutembela magari ya kifahari..ukiachilia utajiri wa magari ya kifahari anayomiliki bondia mwenye utajiri mkubwa Floyd Mayweather ..wapo mastaa wa soka ambao nao wameingia kwenye list ya kutembelea magari ya kifahari zaidi. Hawa ni mastaa 10 wa soka Ulaya ambao mbali ya kuingiza mkwanja mrefu kupitia kazi yao ya soka pia wanatembelea magari ya kifahari…. Gari aina ya  Buggati Veyron  anayomiliki staa wa soka duniani Christiano Ronaldo..gharama yake ni dola 1,7000,000 Ronaldinho anamiliki gari aina ya  Buggati Veyron  yenye thamani ya dola 1,800,000 Eto’o ni mpenzi wa magari na amekua akimiliki magari mengi ya kifahari.. naye pia ni mmoja wa mastaa wanaomiliki gari aina ya Buggati Veyron Zlatan Ibrahimovic anamiliki gari aina ya  Porsche  ambayo ina thamani ya €768,000 Neymar Dos Santos ndiye mchezaji ghali zaidi Brazil: anamiliki gari aina ya  Audi R8 GT  lenye thamani ya paundi 246,000 Mesut Özil a

Ali Kiba kayajibu matano, ishu ya beef, ubalozi wake, Tuzo sita, yeye na Diamond..

Staa wa hits za ‘ Cheketua ‘  na ‘ Mwana’  ambazo zilimrudisha kwa nguvu kwenye muziki TZ,  Ali Kiba   alikuwa kwenye show ya XXL leo July 09 2015, kuna vitu vingi vinaendelea, leo kapata nafasi kuyajibu  haya matano. Ali Kiba   na  B12  kwenye XXL leo mchana. Hivi ndio alivyoupata mchongo wa kuwa Balozi wa Kampeni ya  WildAid  >>> “ Wanaangalia mtu ambaye anaeleweka, anayeweza kuwaambia watu wakaelewa jinsi ya kuzuia ujangili..  Lupita  ni mfano, tayari amekuwa staa mkubwa sana watu wengi wanamuangalia ” Ali Kiba   akisalimiana na  Lupita Nyong’o Haya ndio majibu yake kuhusu sababu za kuamua kufanya  daladala tour  >>> “ Nina imani kuna wanaonipenda na hawajawahi kuniona.. walipiga kura Tuzo za Watu, KTMA.. nilianzia Mnazi Mmoja mpaka Mtoni Mtongani, tukaenda Temeke, tukaja Ilala, Magomeni, Ubungo na Manzese mpaka Makumbusho  ” Maswali yalioulizwa zaidi na watu ndani ya daladala yalihusu nini? >>> “ Iliulizwa kama nina beef na Diamond, ponge

Sikiliza jinsi Diamond Platnumz alivyoguswa na hotuba ya Rais Kikwete

. Baada  ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kulianga rasmi bunge mjini Dodoma msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz ameguswa na hotuba hiyo. Diamond Platnumz ameamplify leo kwenye AMPLIFAYA na kusema’ Kipindi ambacho nimebahatika kumuona Mheshimiwa madaraka na vitu ambacho amevifanya kiukweli ni vitu ambavyo vinagusa sana hususa katika tasnia ya kwetu ya muziki unajua hatujawahi kupata mheshimiwa ambaye akawa anatizama suala la muziki na kulithamini kama la kwake kabisa sio tu suala la muziki na vitu vingi sana mimi sio mtu wa kusikiliza masuala ya siasa wala kuangalia masuala ya kisiasa ‘ – Diamond Platnumz . ‘Leo kwa Mara ya kwanza nilikuwa naendesha gari huku nasikiliza vitu mwanzo mpaka mwisho kuna vitu ambacho alikuwa anazungumza vinagusa moyoni kabisa kuna vitu alikuwa anaongea vya kuchekesha lakini kuna time nilikuwa nafikiri Je rais atakaekuja atakuaje atakuwa kweli anakumbuka jamii yake ukizungumzia kama wasanii

GENERAL NEWS Hii ni Hotuba yote ya Rais Kikwete toka Dodoma July 09 2015 na nukuu ya kile alichokisema

Shughuli ya kwanza iliyompeleka Dodoma  Rais Kikwete   Dodoma ameikalimilisha leo July 09 2015, ilikuwa alihutubie Bunge pamoja na kulivunja Bunge hilo ambapo Wabunge wanarudi Majimboni kwa ajili yakuendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa October 2015. Hotuba yake imechukua zaidi ya saa mbili, najua kuna waliopitwa na hii, na rekodi yote ipo hapa  na unaweza kuisikiliza hapa ........

Mbunge wa CHADEMA kanusurika kwenye ajali ya hii Helicopter leo July 07 2015.

Taarifa ilianza kuenea jioni ya July 07 2015 kwenye kuhusu ajali ya Helicopter iliyokua imebeba Wanachadema mbalimbali akiwemo mbunge Arumeru Mashariki Joshua Nassari. Kwenye ukurasa wa Twitter wa CHADEMA zimewekwa post kwamba Mbunge Joshua Nassari ndiye aliyepata ajali hiyo ya Helicopter, amepelekwa Hospitali kwa ajili ya matibabu pamoja na rubani na watu wengine ambao hawajatajwa, ni baada ya kunusurika. Moshono media inaendelea kufatilia zaidi na chochote kitakachopatikana iwe usiku au mchana utakipata hapahapa.   Mkiti Mbowe ametoa pole, kuwatakia uponaji wa haraka majeruhi wote; Mbunge, viongozi wa chama na rubani @jjmnyika @halimamdee @salum_mwalimu — CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) July 7, 2015 “Tukiwa kikaoni tumepokea taarifa za ajali ya chopper ikiwahusisha Mbunge, Viongozi wa Chama na rubani,” @jjmnyika @halimamdee @JoeMugasa — CHADEMA MEDIA (@ChademaMedia) July 7, 2015 Ni jambo la kumshukuru Mungu Mh.Nassari amenusurika kwenye Ajali hii Mbaya

OKOA MAONO YAKO

Jumapili, 5 Julai 2015 OKOA MAONO YAKO - Maono ni taarifa inayokuja kwa mtu katika hali ya ukamilifu. - Maono ya wakristo waamini walio wengi yamezama yaani yamepoteza mwelekeo, kwa sababu wakristo sana sana jamii ya waaminio hawaweki bidii ya kuishi maisha ya ukweli.  - kila mwanadamu mwenye mwili Mungu amempa kipawa yaani karama, katika hili kinacho leta shida ni wakristo kutokuweka bidii ya kuchochea karama zao, mara nyingi jambo hili husababisha kina cha maarifa ya rohoni kujifunga na hapo huwa ndio mwanzo wa Maono ya mkristo kuzimika. - ( Kinacho linda Maono ya mkristo ni bidii aliyonayo katika kujifunza Neno la Mungu )  - Mkristo anaye mcha Mungu katika hali ya maono mara nyingi safari yake huwa salama kwa sababu maono ni mwongozo sahihi katika maisha ya mtu anaye mwamini Mungu. - ( Kanisa linahitaji maono ili Liwe salama ) - Ili niweze kuyafikia maono yangu inatakiwa nipingane na mambo yafuatayo katika maisha yangu:-   i).Nisi

Ally Nipishe kaipokea zawadi ya gari? maneno yake ni haya kwa Soudy Brown.. #UHeard

Staa wa Bongo Fleva  Ally Nipishe   alisimulia wiki iliyopita kuhusu kisa cha kukamatwa kwake na kuwekwa ndani kwa miezi mitatu baada ya kununua gari ambayo ilikuwa ya wizi. Soudy Brown  leo kamwandalia surprise, dada mmoja kajitolea kumnunulia  Ally Nipishe gari ili kumfuta machozi msanii huyo lakini mwenyewe alikataa kabisa kuipokea zawadi hiyo. Ally Nipishe  alishangazwa na surprise hiyo, huyu dada anasema yeye ni shabiki yake tu, kaguswa na matatizo yaliyompata  Ally  akaona amnunulie gari kumpunguzia machungu ya tatizo ambalo liliwahi kumkuta staa huyo. U Heard iko hapa, sikiliza ilivyokuwa wakati  Ally Nipishe  anataka kupewa zawadi hiyo

Drogba kawataja hawa mabeki kwamba ndio waliomsumbua zaidi Uwanjani..

Didier Drogba Gwiji wa zamani wa soka la kimataifa wa  Ivory Coast  na klabu ya  Chelsea,  Didier Drogba , ni mmoja wa washambuliaji bora zaidi waliowahi kutamba katika barani Afrika, Asia na Ulaya. Drogba  ambaye alitangaza kustaafu kuichezea  Ivory Coast  mwaka jana, pamoja kufahamika kuwa mwiba mkali kwa mabeki wa timu pinzani wakati akiwa kwenye ubora wake,  Drogba   pia nae alikuwa na mabeki ambao walikuwa ni visiki zaidi kila alipokuwa anakutana nao. Didier Drogba   amemtaja nahodha wa zamani wa  Barcelona  na timu ya taifa ya Spain, Carles Puyol ,  Rio Ferdinand , na  Nemanja Vidic  kuwa ndio mabeki visiki zaidi aliowahi kukutana nao. Akizungumza katika mahojiano yake na  Rio Ferdinand ,  Didier Drogba  alisema. “ Siku zote nimekuwa nikisema wewe  Rio  na  Vidic  ni walinzi ambao nilikuwa napata sana taabu timu zetu zinapokutana… Nilipokuwa nikifunga dhidi ya  Manchester United nilikuwa nafurahia sana kwa sababu si mara nyingi nilikuwa nikipata nafasi ya kufunga dhidi

Baada ya Mapenzi au Pesa, Nay wa Mitego kaachia hii nyingine ‘Sina Muda’…(Audio)

Baada ya  Nay wa Mitego  kutoa ngoma yake ya ‘ Mapenzi au Pesa’   akimshirikisha Diamond,  sasa amerudi tena na single nyingine inayojulikana kwa jina la ‘ Sina Muda’. Isikilize hapa mtu wangu…

Majibu ya Diamond Platnumz kuhusu beef, uchawi, kulipia collabo, Team za mitandaoni.. (Audio)

Diamond Platnumz  alikuwa live kwenye XXL @ CloudsFM , kuna vingi kaviongea Exclusive, nilipata nafasi kumsikiliza na hivi ni baadhi ya vitu alivyoviongelea leo June 6 2015. Unadhani   Diamond   anaamini uchawi >>> “ Japokuwa vitabu vya dini vinasema ‘ndele’ zipo lakini  haupaswi kuamini… Kuamini ni sawa na kumkiuka Mwenyezi MUNGU ”>>> Kuna beef kati yake na  Ali Kiba ? Na vipi zile Team kwenye Mitandao ya Kijamii >>> “ Sijawahi kuwa na beef nae hata siku moja… Sioni kama kuna ubaya wowote, kila mtu ana maamuzi kumchagua mtu anayemtaka yeye kumshabikia, huwezi kumlazimisha mtu ” >>> Wawachukue msanii fulani na msanii fulani wawashindanishe na wasanii wa nje, ukiwashindanisha wasanii wa Tanzania haiwezi kusaidia Industry yetu. Kuna malipo ya collabo >>> “ Sijawahi kufanya malipo kufanya nyimbo na mtu yoyote.. Mwanzoni ilikuwa tabu, sasahivi wanafahamu kwamba kufanya nyimbo na Diamond inakuwa rahisi nyimbo kufahamika East Africa…

Tazama na kusiliza Walichokisema Wanasheria na Grey Mgonja baada ya hukumu ya Kisutu leo July 06 2015

>>> “ Washtakiwa wawili wa Kwanza na wa pili wamekutwa na hatia… Mahakama imewaona na hatia, makosa la kwanza mpaka la kumi ilikuwa ni matumizi mabaya ya madaraka. Mgonja Mahakama imemweona hana hatia ” >>> Tumaniel Kweka , Wakili wa Serikali. “ Hatujaridhika.. Hili shauri limesikilizwa na Mawakili watatu, Kama tunaamini uamuzi uliotolewa hauendani na Sheria tutakata rufaa tutakwenda kwenye Mahakama ya juu tutatafsiri Sheria upya “>>> Haya ndio maneno aliyoyasema  Grey Mgonja  nje ya  Mahakama ya Kisutu  baada ya kuachiwa huru>>> “ Hizo zote ni rehema za MUNGU, hakuna mtu mwingine anayeweza… ninaweza kusema hayo tu kwa sasa ” >>>

Tazama Picha kutoka Mahakama ya Kisutu wakati inasomwa hukumu ya Mawaziri wa zamani, Daniel Yona na Basil Mramba

Kesi iliyokuwa inawakabili  Basil Mramba ,  Daniel Yona  na  Agrey Mgonja  kuhusu matumizi mabaya ya madaraka imetolewa hukumu leo katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam. Daniel Yona  na  Basil Mramba  wamehukumiwa  kifungo cha miaka mitatu na faini ya Milioni tano kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya makosa 11,  Grey Mgonja ameachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia. Basil Mramba ,  Daniel Yona   na  Grey Mgonja  wakiwa nje ya mahakama ya Kisutu kusubiri kuingia ndani Familia ya  Daniel Yona  na  Basil Mramba  wakiingia Mahakamani Daniel Yona  akiagana na rafiki zake Basil Mramba   akiingia ndani ya Gari ya Polisi kuelekea gerezani. Daniel Yona  akiingia ndani ya gari ya Polisi kuelekea Gerezani. Gari ya polisi iliyobeba watuhumiwa ikitoka nje ya Mahakama ya Kisutu.