Skip to main content

Posts

Showing posts from April 21, 2013

RAISI KIKWETE ASAMEHE WAFUNGWA 40000

Rais Jakaya Kikwete jana aliongoza maelfu ya Watanzania katika maadhimisho ya miaka 49 ya muungano yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na baadaye kusamehe wafungwa 4,180. Idadi kubwa ya watanzania walishiriki katika maadhimisho hayo hayo ambayo yalianza saa 2:30 asubuhi na kupambwa na gwaride rasmi lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama na kupendezeshwa na halaiki ya wanafunzi 2,695 kutoka Tanzania Bara na Visiwani waliofanya maonyesho mbalimbali ya kuashiria maadhimisho ya muungano. Viongozi mbalimbali wakiwamo wastaafu kutoka Tanzania Bara na Visiwani walishiriki kwenye maadhimisho hayo ikiwa ni ishara ya kuuenzi na kuulinda muungano huo. Viongozi hao ni pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Idd. Wengine wa

HAYA NDO MAKOSA MATATU YALIYOMFANYA GODBLESS LEMA ANYIMWE DHAMANA JANA JIONI

HAYA NDO MAKOSA MATATU YALIYOMFANYA GODBLESS LEMA ANYIMWE DHAMANA JANA JIONI Mambo yaliyomfanya Mbunge wa arusha Godbless Lema akamatwe na kunyimwa dhamana jana jioni ni haya yafuatayo baada ya kuongea na Mwanasheria wa Lema wakili Humphrey Mtui i)Kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa(Worth fighting for) ii)Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off. Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’Kwa hiyo huo ni uchochezi iii)Kosa la Tatu ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisin

RUFAA YA KESI YA ZOMBE YAKWAMA

Mahakama ya Rufani Tanzania imekwama kusikiliza rufaa ya Mkuu wa Upelelezi wa zamani wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na wenzake wanane baada ya kubaini kuwapo kwa kasoro kwenye taarifa ya rufaa hiyo. Haikuelezwa ni lini shauri hilo litasikilizwa. Zombe na watuhumiwa wengine walihudhuria mahakamani hapo. Kutokana na hali hiyo Jamhuri imeomba iruhusiwe kufanya marekebisho, lakini upande wa utetezi umepinga na kuiomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa hiyo. Baada ya upande wa utetezi kutoa msimamo huo sasa mahakama hiyo itatoa uamuzi siku nyingine. Rufaa hiyo iliyokatwa na Serikali kupinga hukumu iliyomwachia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, ACP Abdallah Zombe na wenzake, inatarajiwa kusikilizwa mfululizo. Katika rufaa ya Zombe, Serikali kupitia Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), ilikata rufani kupinga hukumu ya kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini wa mkoani Morogoro na dereva teksi il

GODBLESS LEMA AIBUKA KIDEDEA...RUFAA YA KESI YAKE IMETUPILIWA MBALI

Rufaa ya kesi ya Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema imetupiliwa mbali na mahakama kumtangaza mbunge huyo kuwa ni halali. Rufaa hiyo ilisikilizwa na majaji watatu wa Mahakama Rufaa Tanzania ambao ni Engili Kileo, Salum Massati na Benard Luanda kwa pamoja wametupilia madai ya rufaa hiyo. Mahakama hiyo imewaamuru tena wakata rufaa walipe gharama zote za kesi.

Katiba mpya na hatma ya Tanzania

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (UDSM) Bashiru Ally Tanzania ipo kwenye kipindi cha mpito: kijamii, kiuchumi na kisiasa. Kila mwenye uwezo wa kutafakari, ana cha kusema kuhusu mustakabali wa taifa hili. Watu wengi, kupitia njia mbalimbali za mawasiliano, wanatoa tafakuri zao kuhusu suala hilo. Mmoja wa watu hao ni Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa katika Chuo kikuu cha Dar es salaam, Bashiru Ally ambaye anasema, “Ninapotazama Tanzania ijayo, ninaona giza totoro. Tofauti na watu wengi, hataki kuzungumzia kasoro zinazojitokeza katika mchakato wa kuunda Katiba mpya, akisema kinachotokea ni matunda ya mbegu zilizopandwa. Akifafanua kauli hiyo, anasema; “Tanzania haikuwahi kuandika Katiba kwa kushirikisha wananchi kwa njia ya moja kwa moja. Kazi hii haiwezi kutekelezwa kwa mara ya kwanza, ndani ya miaka miwili mpaka mitatu na endapo hilo litatokea, yatakuwa maajabu ya dunia.” Mtaalamu huyo wa masuala ya siasa nchini anasema, taifa limegawanyika kisiasana kimatabaka. Wan

Serikali yafunga viwanda vya nondo

Inspekta wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Yona Afrika akizugumza na Meneja wa Kiwanda cha nondo cha Metro cha jijini Dar es Salaam, Onesmo Ngondo mara baada ya TBS kukifungia kiwanda hicho kwa muda usiojulikana , kutokana na kuzalisha nondo zisizo na viwango vya ubora vinavyotakiwa. Picha na Beatrice Moses                                         Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limevifungia viwanda viwili vya kuzalisha nondo kwa muda usiojulikana. Viwanda vilivyofungiwa ni vya Metro Steel Mills kilichoko Vingunguti Dar es Salaam na Quaim Steel Milis kilichopo Chang’ombe wilayani Temeke. Hatua hiyo imekuja baada ya kubainika kwamba vimekuwa vikizalisha na kuuza nondo zisizo na ubora wa viwango vinavyokubalika na hivyo kuwa tishio kwa watumiaji wa bidhaa hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Quaim, Hassan Amir, alisema kiwanda chake kilianza kuzalisha nondo tangu mwaka 2006. Katika maelezo yake, , alipinga hatua hiyo ya TBS akidai kwamba inafanywa kinyume c

CHADEMA NA CCM NI MAKOMBORA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Fire, Morogoro jana. Picha na Wapigapicha Wetu Mwanza. Wabunge sita wa Chadema waliosimamishwa bungeni wameamua kwenda kuwashtaki Spika Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai kwenye majimbo yao. Wakitangaza uamuzi huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi ya Mbugani, Mwanza jana, walisema pia watakwenda kwenye majimbo ya wabunge wawili wa CCM, Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi) na Livingstone Lusinde (Mtera) ili kueleza jinsi wabunge wa upinzani wanavyokandamizwa bungeni Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Ezekiah Wenje (Nyamagana).

BEEF YA BEN PO NA LADY JAY DEE YAMALIZWA NA NGOMA MPYA YA BEN PO.......JIKUBALI ITAYOTOKA TAREHE 30 MWEZI HUU

  BEEF YA BEN PO NA LADY JAY DEE YAMALIZWA NA NGOMA MPYA YA BEN PO.......JIKUBALI ITAYOTOKA TAREHE 30 MWEZI HUU           Hatimaye Lile bifu la Lady Lady J Dee na Ben Po ambapo walitofautiana kauli hadi kuharibiana kwenye Mtandao wa kijamii wa twitter leo imeisha rasmi. Leo msanii ben Po ameachia studio tears ya ngoma yake mpya ambayo inafuata inayokwenda kwa jina la Jikubali ngoma ambayo pia ameitaja kuwa inatoka tarehe 30 mwezi huu yaani mkesha wa Kuamkia may mosi basi katika ngoma hiyo na studio tears aliyoiachia inaskika akiimba nampenda lady jay Dee wakati tayari wako kwenye beef kitu ambacho amefunguka na kusema kuwa yeye aliurecord wimbo huo kabla hawajaingia kwenye malumbano na JD ila ameona haina haja ya kuuedit wimbo huo kwani kiukweli anampenda Jd na kufunguka kuwa yeye hawezi kuwa na beef na JD kwani Jide ni msanii mkubwa sana na yeye pia anatamani kukubalika kama JD. JD BEN PO amefunguka na kusema kuwa walitofautiana tu

MPENZI WANGU HUWA ANATOKWA NA HAJA KUBWA WAKATI WA TENDO".....HAYA NDO MAJIBU YA UCHUNGUZI BAADA YA KUOMBA USHAURI

Hivi karibuni tuliweka habari ya mdau aliyekuwa anaomba ushauri kuhusu mpenzi wake ambaye alikuwa anatoa haja kubwa wakati wa tendo...... Pamoja na jitihada za kumuuliza kama ni mdau wa 0718 ,binti huyo aligoma kabisa na ndipo jamaa alipoamua kufanya uchunguzi wa chinichini na kubaini ukweli HILI NI SIMULIZI LAKE: ----------- Kwanza nawashukuru sana kwa maoni, mitazamo na ushauri wenu juu ya tatizo langu nililolitoa siku chache zilizopita..... Baada ya kupitia maoni mengi niliamua kutumia ujanja na nguvu ya ziada ili niupate ukweli ulikokuwa umejificha... Jana mida ya saa 1 usiku niliamua kutoka out na huu mpenzi wangu ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuuu.Lengo lilikuwa ni kumnunulia pombe nyingi alewe ili nione kama kuna siri yoyote naweza nikaigundua toka kwake... Kwa kuwa mimi huwa situmii pombe ,niliamua kumuita na rafiki yangu na mpenzi wake waje kunipa support,hivyo tukawa

LULU MICHAEL "FAKE" ABEMBELEZA MASTAA WAMFOLLOW TWITTER

Inaonekana muigizaji wa filamu Elizabeth ‘Lulu’ Michael ameingia location kufanya filamu yake inayoaminika kuwa ya kwanza tangu atoke mahabusu mwezi January mwaka huu. Kupitia Instagram, juzi Lulu ameshare picha inayomuonesha akiwa location na muigizaji Hashimu Kambi na kuandika, take 1 action, Mic location, me doing my thng.” Katika hatua nyingine, Lulu amelalamika kuwepo kwa akaunti fake ya Twitter yenye jina lake iitwayo @Lulu_actress. “Haya lulu mwingne huyo on twitter…..!am tired jaman…nyie ma lulu nioneeni huruma basi…..!!!nimechoka kusikia case’z zenu!!!!NIMECHOKA JAMANI ,” ameandika Lulu kupitia Instagram. Katika akaunti hiyo Fake, mtu huyo ameandika profile yake isemayo: Am a bongo movie actress|caring,loving and loved lady| latest movie coming soon by the name The end of tourture| starring wil be me and jb Akaunti halisi ya Lulu kwenye mtandao wa Twitter ni ile yenye jina @hotlulumichael.

hizi hapa picha za Prezzo akiwa mtupu na mademu!

PREZZO AUMBULIWA NA PICHA ZAKE ZA UTUPU Jackson Makini a.k.a. Prezzo is in trouble…..on Saturday after the release of his new and controversial track Liqher, his n*ked photos enjoying some private time with two lasses were leaked to the internet. Source:Daily post

WANAWAKE WAUNGANA KUSUSIA BIDHAA NA MAONYESHO YA MWANAMUZIKI DIAMOND

Kwa Kumdhalilisha Bi.Wema Sepetu kwa kumrekodi katika simu na kusambaza mazungumzo nyeti ! Kitendo cha Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond,cha kurekodi mazungumzo yake na star wa Bongo Move Bi.Wema Sepetu, na kuyatuma mazungumzo yao ya mapenzi katika mitandao ni kitendo cha "Udhalilishaji wa Mwanamke" . kwa kuwa wanamuziki na wasanii wote wanatakiwa wawe ni mfumo na kioo cha jamii katika kuielekeza jamii kuishi kwa kufuata na kuheshimu maadili ,lakini mwanamuziki Diamond ameonekana kuwa ni kiongozi wa " Udhalilishaji wa Mwanamke" kufuatia kitendo chake cha kurekodi na kusambaza mazungumzo yao ya simu ya kimapaenzi kati yake na Bi.Wema Sepetu na mpenzi wake wa sasa Bi.Penny,kitendo hiki ni cha " kuwadhalilisha wanawake wa kitanzania" Tunaowaomba akinamama na kinadada na wanawake wote kwa ujumla kususia kununua video,vcd,cd pia kugomea kuhudhuria onyesho lolote lile litakalofanywa na mwamuziki Na

hawa ndio wanaume walio tembea na Baby Madaha!

AWAMU HII NITAWAPANGA WANAUME KAMA MAGUNIA....MBONA HATA WAO HUTUCHEZEA"....BABY MADAHA STAA wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amesema mwaka huu atawachanganya wanaume kama afanyavyo Nasibu Abdul ‘Diamond’ ili kwenda sawa. Akifafanua kauli yake kwa mwandishi wetu, Baby Madaha aliweka bayana kuwa haoni tatizo kunaswa na Mwisho Mwampamba kama ilivyoripotiwa hivi karibuni wakati huohuo anatoka kisela na mkali wa Bongo Fleva, Juma Kassim ‘Nature’. “Watakoma mwaka huu, lazima niwachanganye sana, mbona wao wanatuchanganya sana kama Diamond vile anavyofanya!” alisema Baby.

huyu hapa Rose Ndauka akifanya mambo ya chumbani hadharanii!

                                                Staa anayefanya poa katika sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka amenaswa akiwa kimahaba akifanya mambo ya chumbani hadharani na mchumba’ke, Malick Bandawe, Ijumaa Wikienda limewapiga chabo.Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu, lilijiri wikiendi katika Ukumbi wa Hazina Lounge uliopo Coco Beach, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya ‘bethidei’ ya mdogo wake Rose, Recho Ndauka.Baada ya kukolea…...                       Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu, lilijiri wikiendi katika Ukumbi wa Hazina Lounge uliopo Coco Beach, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya ‘bethidei’ ya mdogo wake Rose, Recho Ndauka.Baada ya kukolea kwa ‘maji’, Rose na mwanda

Je wajua Darasa la saba sasa kujiunga vyuo vikuu?

      Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao. Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu. ... Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B. Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu. Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning’ (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.

TAPELI ANAYETUMIA JINA LA WAZIRI LUKUVI AMTAPELI LOWASSA IRINGA

 maofisa wa polisi mkoa wa Iringa wakiweka mtego katika nje ya ukumbi wa St Dominic ili kumnasa tapeli huyo anayejiita ni mtoto wa waziri Lukuvi na kutapeli watu Tapeli anayetapeli watu maeneo mbali mbali ya Tanzania kupitia jina la waziri Lukuvi akiingizwa ktk gari maalum leo Tapeli Jonathan Wiliam Lukuvi feki akitiwa matatani askari kanzu Iringa Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma ,askofu Dkt Boaz Sollo na Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa akimsikiliza tapeli huyo akimpa maneno ya kitapeli Lowassa Kijana huyo Tapeli akimsomesha waziri Lowassa ukumbini kwa kuahidi kuchangia 100,000 huku akimwomba kumsaidia misaada zaidi Hapa akipelekwa katika gari maalum Hapa akiingizwa katika Taxi tayari kwenda polisi Kijana ambae amekuwa akiwaliza watumishi mbali mbali wa umma na watu binafsi kwa kutumia jina la waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge kijana Jonathan Wiliam L

Hii ndio hali halisi ya elimu nchini

Madai kuwa kiwango cha elimu nchini kimeporomoka yametawala katika ndimi za wadau wengi wa elimu. Matokeo mabaya ya mitihani hasa ile ya Taifa imekuwa ikitumika kama hoja mojawapo ya kushadadia hali hiyo. Upi ukweli kuhusu kiwango cha elimu yetu? Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa anaelezea hali halisi ya elimu nchini kama alivyohojiwa na mwandishi wetu . Swali: Serikali imejipanga vipi kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa kwa Watanzania ni bora? Jibu: Ili kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa kwa Watanzania ni bora, Serikali imepanga kufanya yafuatayo katika mwaka wa fedha 2013/14: Kwanza, kuinua ubora wa elimu katika ngazi zote za elimu kwa kuongeza idadi ya walimu na wakufunzi na hasa walimu wa masomo ya Sayansi, Hisabati, Teknolojia na Lugha katika ngazi ya elimu ya msingi na sekondari; kutoa mafunzo ya kuongeza ufanisi katika ufundishaji na kujifunza kwa walimu ikiwa pamoja na kuimarisha stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu; kuendesha na kuonge

Chadema ‘waitupia kombora’ Idara ya Usalama wa Taifa

            Katika hotuba hiyo iliyohaririwa, Profesa Kahigi alisema baadhi ya maofisa wa idara hiyo wamekuwa wakitajwa kwenye vyombo vya habari kuhusika na uhalifu huo, lakini Serikali imekaa kimya. Wasema inajihusisha kwenye vitendo vya utekaji na utesaji watu wanaoikosoa Serikali Kambi Upinzani Bungeni imeitaka Serikali kuwachukulia hatua maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa – Ikulu ambao wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu vya utekaji na utesaji kwa watu wanaoonekana kuikosoa Serikali. Madai hayo yalitolewa bungeni juzi na msemaji wa kambi hiyo, kuhusu Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Profesa Kulikoyela Kahigi, katika hotuba ambayo awali ilizua mvutano wa mambo gani yasomwe na yapi yabaki. Ilibidi hotuba hiyo iahirishwe kwa muda, hadi kamati ya kanuni ikutane na kutoa uamuzi kwamba baadhi ya mambo yanayotaja majina ya watumishi wa usalama wa taifa na mengine yaliyoko mahakamani yaondolewe. Katika hotuba hiyo iliy

HIZI HAPA SABABU ZINAZOSABABISHA MTU KULIA MACHOZI!

                            Unaitazama filamu ya msanii Kanumba. Wewe pamoja na wenzako mnatiririkwa na machozi yanayoambatana na kwikwi.   Ghafla unatazama pembeni, unamwona paka wako akikushangaa kwa kilio chako ambacho kinatokana na tukio la filamu ambalo ni la kufikirika tu. Unafikiri ni kwa nini binadamu analia akiwa mtoto mchanga hadi anapokuwa mtu mzima tofauti na wanyama wengine? Wanasayansi waeleza Watafiti wa nchini Ujerumani walifanya utafiti kuhusu kulia na kubaini kuwa wanawake hulia kati ya mara 30 hadi 63 kwa mwaka na wanaume hulia mara 6 hadi 17 kwa mwaka. Wanaume hulia kwa dakika mbili hadi nne wakati wanawake hulia kwa zaidi ya dakika sita. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili, Dk Kitila Mkumbo anasema kitendo cha kulia kinatokana na mifumo ya hisia. Anasema binadamu huweza kulia kutokana na hasira, maumivu au furaha. Zipo aina tatu za machozi Binadamu yeyote ana mirija ya machozi ambayo hutumika kulowanisha na kulinda macho yas

JE WAJUA? DAWA YA KUONGEZA AKILI HII HAPA!!

JE WAJUA? DAWA YA KUONGEZA AKILI HII HAPA!! Mtindo wa maisha, ulaji na msongo wa mawazo, vimewasababishia Watanzani wengi maradhi lukuki hata vifo. Hata hivyo, wataalamu wa afya kutoka Afrika Kusini wamekuja na dawa maalumu, zilizo na uwezo wa kurudisha kumbukumbu, kuongeza upeo darasani, kuondoa sumu mwilini na kumfanya mzee kuonekana kijana. Dawa hizo zinazotumia vitamini zilizomo kwenye vyakula vya kila siku, zina uwezo wa kuongeza kiwango cha uelewa kwa mwanafunzi au mfanyakazi. Kiwango hicho cha uelewa kitaalamu unatambulika kama ‘IQ’. Mratibu wa dawa hizo hapa nchini, John Haule anasema kuwa dawa hizo zina uwezo wa kufanya kazi kwa haraka. “Virutubisho hivi ni vizuri kwa wale wanaokwenda katika mitihani au wanataka kufanya kazi inayohitaji umakini wa hali ya juu,” anasema Haule na kuongeza: “Zimetengenezwa kwa vyakula tunavyotumia na siyo kemikali.” Haule ambaye ni mtaalamu wa tiba asili na mimea anasema kwamba mtindo wa maisha na