Skip to main content

RUFAA YA KESI YA ZOMBE YAKWAMA


Mahakama ya Rufani Tanzania imekwama kusikiliza rufaa ya Mkuu wa Upelelezi wa zamani wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na wenzake wanane baada ya kubaini kuwapo kwa kasoro kwenye taarifa ya rufaa hiyo.

Haikuelezwa ni lini shauri hilo litasikilizwa.

Zombe na watuhumiwa wengine walihudhuria mahakamani hapo.

Kutokana na hali hiyo Jamhuri imeomba iruhusiwe kufanya marekebisho, lakini upande wa utetezi umepinga na kuiomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa hiyo.

Baada ya upande wa utetezi kutoa msimamo huo sasa mahakama hiyo itatoa uamuzi siku nyingine.

Rufaa hiyo iliyokatwa na Serikali kupinga hukumu iliyomwachia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, ACP Abdallah Zombe na wenzake, inatarajiwa kusikilizwa mfululizo.

Katika rufaa ya Zombe, Serikali kupitia Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), ilikata rufani kupinga hukumu ya kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini wa mkoani Morogoro na dereva teksi iliyokuwa ikimkabili Zombe na wenzake.

Hukumu hiyo, ilitolewa Agosti 17, mwaka 2008 na Jaji Salum Massati wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, ambaye aliwaachia huru washitakiwa wote na kuuamuru upande wa Jamhuri kuwatafuta wahusika wa mauaji hayo.

Kwa mujibu wa ratiba za vikao ya Mahakama ya Rufani, rufaa hiyo imepangwa kusikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu, Edward Rutakangwa, Jaji Mbarouk Mbarouk na Jaji Bernard Luanda.

Mbali na Zombe, wajibu rufani wengine ni askari polisi Christopher Bageni, Ahmed Makele, Jane Andrew, Koplo Emmanuel Mabula, Michael Shonza, Abeneth Saro, Rajabu Bakari na Festus Gwasab.

Zombe na wenzake, walikuwa wakidaiwa kuwa Januari 14, mwaka 2006, waliwaua wafanyabiashara watatu wa madini wa wilayani Ulanga, mkoani Morogoro; Ephraim Chigumbi, Sabinus Chigumbi na Mathias Lukombe pamoja na dereva teksi Juma Ndugu, mkazi wa Dar es Salaam.

Katika hukumu hiyo, Jaji Massati alisema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa, bila kuacha shaka yoyote na hivyo mahakama hiyo inawaona washitakiwa hawana hatia na inawaachia huru.

Alisema mahakama hiyo, imebaini wauaji halisi hawajafikishwa mahakamani hivyo kutokana na kutokuwepo kwao, mashitaka dhidi ya washitakiwa hayawezi kutengenezeka, aliuagiza upande wa Jamhuri uwasake na kuwafikisha mahakamani wahusika.

Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, DPP aliamua kwenda Mahakama ya Rufani, kukata rufani iliyosajiliwa na kupewa namba 254/2009, kupinga hukumu hiyo kwa madai ya kwamba hajaridhika nayo.

Katika rufani hiyo, DPP aliwasilisha hoja 11 za kisheria kupinga hukumu hiyo, akidai kwamba kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani, washitakiwa wote walikuwa na hatia.

Miongoni mwa sababu nyingine, DPP anadai kulikuwa na upungufu katika hukumu hiyo kwa kila mshtakiwa.

DPP, anadai Jaji Massati alipotoka na kushindwa kutafsiri sheria pamoja na kanuni mbalimbali zinazohusu mashtaka ya jinai na kwamba alijichanganya sana katika hukumu hiyo.

Alidai kushangazwa na Jaji Massati kushindwa kuwatia hatiani washitakiwa wote, licha ya kwamba kulikuwa na ushahidi wa dhahiri na kimazingira wa kutosha kuwatia hatiani.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...