Skip to main content

Posts

Showing posts from June 14, 2015

Fastjet yafadhili ziara ya waandishi wa habari wa Tanzania nchini Zimbabwe

Pichani ni Mhudumu wa Mapango ya  Chinhoyi Cephas Sithole akitoa maelezo kwa timu ya waandishi wa habari waliombatana na wadau wa utalii kutoka nchini Afrika Kusini kwenye ziara hiyo ya kutembelea vivutio vya utalii nchini Zimbabwe katika mapango Chinhoyi.(Picha zote na Zainul Mzige). Na  Modewjiblog  team, Harare Waandishi wa habari kutoka vyombo 5 vya habari vya magazeti ya Tanzania ikiwemo mtandao wa habari wa modewjiblog ambao ni Justin Damiana (The African), Frank Aman (The Guardian), Zainul Mzige ( modewjiblog ), Mariam Said (Daily News) pamoja na Timothy Kitundu (East Africa Business Week) walipata mwaliko kutoka Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA) kufanya utalii katika mapango ya Chinhoyi, Ziwa Kariba, Shamba la ufagaji wa Mamba, Hifadhi ya Taifa ya Kariba, Bandari ya Zambezi pamoja na ukuta wa bwawa la Kariba unaotengenisha nchi ya Zambia na Zimbabwe. Safari ya kuelekea nchini Zimbabwe ilidhaminiwa na Shirika la usafiri wa Anga wenye gharama nafuu Fastje