Skip to main content

Posts

Showing posts from October 20, 2013

DK. SHEIN AKIWA NA MMZUNGUMZO NA WAANDISHI WA HABARI LEO

ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na Kamati ya uandishi wa taarifa za Serikali,katika mahojiano maalum kuhusu maendeleo ya Zanzibar,ikiwa ni katika  maadhimisho   ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo mchana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Kamati ya uandishi wa taarifa za Serikali,katika mahojiano maalum kuhusu maendeleo ya Zanzibar,ikiwa ni katika  maadhimisho   ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo mchana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] WATALII MBALIMBALI NDANI NA NJE YA NCHI WATAKIWA KUTANGAZA UTALII by  JOHN BUKUKU  on  OCTOBER 24, 2013  in   BIASHARA   with   NO COMMENTS Washindi wa shindano la Biggest Baddiest Bascket, Allex Ayling (kushoto) na Mwenzake Mark wakitembezwa na kuangalia namna walemavu wa kituo cha  Shanga

Baby Madaha afanya mazito Kenya, jionee hapa! Hatari Sana!

Mwanadada aliyerudi kwa kasi kwenye gemu la muziki nchini na kuachia ngoma zake mbili kali sana mwaka huu “ Squeeze it ” na “ Summer Holiday ”, Baby madaha, ameendelea kudhihirisha kuwa mwaka huu kajipanga Zaidi kusaka hela baada ya hivi karibuni kuachia Perfume na Mifuko yenye jina lake (Brand) huko nchini Kenya. Akizungumza kwa simu tokea nchini humo ambako yupo akijiindaa kufanya tour yake ya kwanza baada ya kupata Mkataba na Kampuni ya Candy n Candy records ya nchini humo, Baby Madaha amsema perfume hizo zimeshaanza kuuzwa na kupatikana katika mitaa na maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na amesema kuwa mzigo wa pili utatua Tanzania hivi karibuni. “Nimeona  bora nianze na Kenya kwanza kwasababu nimegundua kuwa huku nina mashabiki wengi sana Zaidi hata ya bongo, hata siamini kinachotokea” Alisema baby Madaha.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA NA KUKAGUA JENGO LA BUNGE MJINI DODOMA LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Oktoba 24, 2013 ametembelea na kukagua Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kujionea maandalizi ya jinsi Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba watakavyokaa katika Ukumbi wa Bunge hilo. Bunge hilo Maalum la Katiba litakuwa na Wabunge 600 tofauti ya Bunge la sasa lenye Wabunge 354 ambao ni pamoja na Wabunge 239 wa kuchaguliwa kutoka majimboni, Wabunge Wanawake Viti Maalumu 102, Wabunge wa kuteuliwa toka Baraza la Wawakilishi Zanzibar 5, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wabunge 7 (kati ya 10) wa kuteuliwa na Rais. katika picha Rais Kikwete akizungumza na Naibu Spika Mhe Job Ndugai na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila baada ya kutembeleaUkumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013 PICHA NA IKULU Rais Kikwete akikaribishwa kutembelea Jengo la Bunge mjini Dodoma na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai leo Oktoba 24, 2013 Rais Kikwete akiangalia sehemu ya viti ndani ya Ukumbi wa  Bu