Skip to main content

Posts

Showing posts from November 29, 2015

Gari la Magazeti ya Mwananchi Lapata Ajali....Wawili Wafariki Dunia Papo Hapo

WATU wawili wamefariki dunia Papo hapo baada ya Gari walilokuwa wakisafiria lililobeba Magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti kwenda mkoani mkoani Mbeya kupata ajali Eneo la Kitonga Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa. Ajali hiyo imetokea leo alfajiri baada ya dereva wa Gari hilo kujinusuru kugongana uso kwa uso na gari jingine, hivyo kulazimika kuingia nyuma ya lori na kupelekea kifo chao. Kwa mujibu wa Wakala Afisa mauzo wa magazeti ya Mwananchi Mkoa wa Iringa Alex Kadea ambae alifika Eneo la tukio ameithibitisha kutokea kwa ajari hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa matukiodaima kuwa waliofariki dunia wote wawili walikuwa ni madereva wa Gari hilo.   chanzo Mpekuzi blog

Tahadhari Kuhusu Kuingilia Au Kufuatilia Mawasiliano Ya Watu

TAARIFA KWA UMMA TAHADHARI KUHUSU KUINGILIA AU KUFUATILIA MAWASILIANO YA WATU *** Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa Programu (Application) ya simu ikijulikana kama SOFTBOX TANZANIA iliyosemekana iko kwenye Google PLAYSTORE. Ilidaiwa kuwa program (Application) hiyo ya SOFTBOX TANZANIA ilikuwa na uwezo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi. Kwa yeyote aliyekuwa na nia hiyo ya kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu mwingine alihitajika kulipia fedha kiasi cha Tshs 35,000/= kupitia mitandao ya simu ili kupata namba ya siri kwa ajili ya kuwezesha nia hiyo. Mamlaka ya Mawasiliano imefanya uchunguzi kubaini kuwepo kwa programu hiyo na ukweli kuhusu uwezo wake wa kufanya kilichodaiwa, ikiwa ni pamoja na kuangalia madhara ya program hiyo na sheria inasema nini kuhusu suala hili.   B

Magufuli Aitaka TRA Kutoa Mashine za EFDs Bure.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ameishangaa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kutogawa bure Mashine za EFDs, na wao kubaki na kazi ya kukusanya mapato. Akizungumza katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji jana jijini Dar es Salaam, ulioandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), alisema muda uliopotea na kodi ambayo haikukusanywa wakati wa mvutano na wafanyabiashara ungetosha kununua mashine mpya na kuwagawia. “Kama mnajua mashine hizi ni halali na ni zenu, wapeni bure kazi yenu iwe ni kukusanya kodi, ni hesabu rahisi sana isiyohitaji kwenda chuo kikuu kuwa muda uliopotea na fedha hazifiki bilioni 12 zingetosha kununua na iwe kazi ni kukusanya kodi,”  alisema. Awali katika salamu zake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Jonson Minja, alimpongeza rais kwa kazi kubwa aliyofanya Bandarini na TRA kwa kuwa imewezesha kodi kukusanywa kwa usahihi na kwamba kipindi cha nyuma fedha nyingi zilipot

Rais Magufuli amteua Valentino Mlowola Kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John P. Magufuli, amemteua Valentino Mlowola, kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU   kuziba nafasi iliyoachwa wazi na  Lilian Mashaka aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kabla ya Uteuzi Mlowola alikuwa ni Kamishna wa Polisi na Mkurugenzi Intelijensia ya Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi. Pia,kabla ya kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi na Mkurugenzi Intelejensia ya Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.

TRA Yakusanya Bilioni 5 za Kodi ya Makontena 329......Wafanyakazi 35 Wasimamishwa Kazi

BAADA ya Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kufanya ziara ya kushitukiza katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kubaini upotevu wa Makontena 329, mapya yaibuka kwa Makampuni 43 kuhusika kukwepa kodi ya Sh.Bilioni 12.6 katika Bandari Kavu inayomilikiwa na Said Salim Bakhressa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa kampuni hizo 43 zilipitishiwa Kontena katika Bandari Kavu ya Said Salim Bakhressa na kutaka ndani ya siku sita kuanzia leo kampuni zote ziwe zimeshalipia kodi kutokana na idadi ya kontena. Dk. Mpango amesema katika kampuni ambazo zilizokwepa kodi ambazo zilipitisha Kontena 329 wameshalipa zaidi ya Sh. Bilioni Tano(5) ambapo wanatakiwa kulipa kodi iliyobaki kuweza kumaliza kodi ya Sh.Bilioni 12.6 kwa kipindi alichoweka Rais Dk .John Pombe Magufuli.  Kampuni zilizokwepa Kodi ya mapato kwa makontena 329 ni Lotai Steel Tanzania LTD yenye makontena 100,Tuff T

Tazama full video ya Rais Magufuli alipokutana na Wafanyabiashara wa Tanzania Ikulu.

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  Dr. John Pombe Magufuli  leo December 3 2015 alikutana na Wafanyabiashara mbalimbali kwenye sekta binafsi ambao kwa siku kadhaa sasa wamekua wakiomba kukutana nae,  bonyeza play  hapa chini kwenye hii video umsikilize  Rais Magufuli  kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Hizi ndio rekodi 5 za soka ambazo hazijawahi kuvunjwa katika historia ya soka

Tukiwa tunaelekea kuuaga mwaka 2015 kuna mengi yametokea katika maisha ya soka, moja kati ya vitu vilivyotokea katika soka mwaka 2015 tumeshuhudia  Jamie Vardy  wa klabu ya  Leicester City   akivunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa klabu ya  Man United   Ruud van Nistelrooy  ya kufunga magoli 10 mfululizo. Rekodi ambayo ilidumu kwa miaka 12 toka  Van Nistelrooy  aiweke. December 5 naomba nikusogezee rekodi za soka ambazo hazijawahi kuvunjwa toka zimewekwa, Stori kutoka  sportskeeda.com  hadi kufikia November 16 2014 ndio zilikuwa rekodi ambazo hazijawahi kuvunjwa katika soka. 1- Idadi ya mashabiki wengi wa soka kuingia uwanjani: Hii ni rekodi iliwekwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la  Dunia  mwaka 1950 katika mchezo kati ya  Brazil  dhidi ya Uruguay  katika dimba la  Maracanazo , mchezo ambao unatajwa kuingiza idadi rasmi ya watu 173,850 ila inatajwa kuwa idadi ilifikia hadi watu 210000 pamoja na wasio kuwa na tiketi. 2- Mechi iliyowahi kufungwa magoli mengi zaidi

HAWA NDIO WATUHUMIWA 8 WA UPOTEVU WA MAKONTENA 349 WAFIKISHWA MAHAKAMANI

KASI ya utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa imeanza kuwagusa baadhi ya watendaji wa Serikali baada ya maofisa wanane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA), akiwemo Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo Tiagi Masamaki (56) kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7 za kitanzania.   Ukimuondoa Masamaki maofisa wengine waliopandishwa kortini ni Habibu Mponezya (45) Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,Bulton Mponezya (51)   Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa akisaidiana na Peter Vitalis  ameadi leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa mawili.   Alidai makosa mawili ya uhujumu uchumi ni kula njama ya kuidanganya Serikali na kuisababishia Serikali hasara. Kesi hiyo ni namba 35/2015 ya uhujumu uchumi.   Ilidaiwa k

SOMA WARAKA WA KUFUTA ADA ELIMU YA SEKONDARI ( KIDATO CHA 1 HADI 4) NA MICHANGO YOTE ELIMU YA MSINGI

Serikali imeamua kutoa elimu pasipo malipo kwa elimumsingi kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne,kuanzia mwaka wa masomo wa 2016. Azima hii ya serikali ni katika kutekeleza sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ina lengo la kuhakikisha kwamba watoto wote wa Tanzania wanapata Elimu bila kikwazo ikiwemo ada au malipo. Katika kutekeleza maamuzi hayo,ada zote zilizokuwa zikilipwa kwa ajili ya elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne zimefutwa.Pia, waraka wa Elimu namba 8 wa mwaka 2011 kuhusu michango shuleni nao pia umefutwa. Aidha, mwongozo wa elimumsingi bila malipo unaandaliwa na utatumwa kwa wamiliki wa shule ifikapo au kabla ya tarehe 15 Disemba 2015. Waraka huu umeanza kutumika tarehe 21 Novemba 2015

Huyu ndiyee AFISA ARDHI MOROGORO KAPEWA SIKU 14 ZA KUJIELEZA KWA NINI ASIFUKUZWE KAZI

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Jumanne Sagini Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Jumanne Sagini ametoa siku 14 kwa Afisa Ardhi, Mhandisi wa Majengo na Afisa Mipango Miji Manispaa ya Morogoro kuandika maelezo ya kwanini wasifukuzwe kazi kutokana na kufanya kazi chini ya kiwango na kukiuka maadili ya utumishi wa umma Agizo hilo limekuja kufuatia watendaji hao wa serikali kutumia vibaya mamlaka waliyopewa na serikali ikiwemo kuruhusu ujenzi wa hoteli ya Flomi iliyopo eneo la Msamvu mjini Morogoro, kujengwa katika eneo ambalo wanajua limepita bomba la mafuta la TAZAMA. Pia kushindwa kuzuia ujenzi wa holela katika maeneo yasiyo rasmi pamoja na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya ofisi hizo. Chanzo -GPL

silkiliza Sentensi nne za DC Paul Makonda alivyomalizana na mgomo kiwanda cha URAFIKI Dar

Hii stori nilikuzogezea muda mfupi uliopita kuhusu ishu ya mgomo wa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha URAFIKI kilichopo eneo la  Shekilango Dar es Salaam . . Updates za taarifa iliyonifikia muda mfupi uliopita ni kwamba Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, DC  Paul Makonda   ameagiza shughuli zote za kiwanda hicho zisimame kwa sasa mpaka mgogoro wa kimaslahi kati ya wafanyakazi na wamiliki wa kiwanda hicho utakapotatuliwa. Hapa nanukuu maneno ya DC  Paul Makonda   mbele ya wafanyakazi hao >>> “ Kwanza wasimamishe shughuli za uzalishaj, hatuwezi kuzalisha kwenye mazingira ambayo hayana amani… ninaenda kumtafuta Katibu Mkuu wa Wizara ili achukue hatua dhidi ya watawala wasio na majibu ya kero za wananchi “- . Sauti ya stori hiyo hii hapa kutoka kwenye habari ya  TBC 1

Tazama Pichaz 14 za Kilimanjaro Stars ilivyowasili uwanja wa ndege wa JKIA Dar baada ya kutolewa Challenge

Timu ya taifa ya  Tanzania  bara  Kilimanjaro Stars  imewasili  Dar Es Salaam  December 2 ikiwa ni siku mbili zimepita toka itolewe na timu ya taifa ya  Ethiopia  katika michuano ya mataifa ya  Afrika Mashariki  na kati maarufu kama  CECAFA Senior Challenge Cup 2015 .  Kilimanjaro Stars  itolewa na  Ethiopia  katika hatua ya robo fainali kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 1-1. Naomba nikusogeze pichaz 15 za timu ya taifa ya  Tanzania  Bara  Kilimanjaro Stars  ikiwasili uwanja wa ndege Dar Es Salaam. Himid Mao baada ya kuwasili Nahodha wa Kilimanjaro Stars John Bocco baada ya kutua Dar akielekea katika basi. John Bocco na kocha mkuu na msaidizi wake wakizungumza jambo Shomari Kapombe ndani ya basi la timu ya Taifa Hassan Kessy akipanda basi la Stars Mshauri wa Kilimanjaro Stars na kocha wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa akisalimia na mdau Simon Msuva akiingia katika gari lake baada ya kuja kupokelewa na mdogo wa