Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Jumanne Sagini ametoa siku 14 kwa Afisa Ardhi, Mhandisi wa Majengo na Afisa Mipango Miji Manispaa ya Morogoro kuandika maelezo ya kwanini wasifukuzwe kazi kutokana na kufanya kazi chini ya kiwango na kukiuka maadili ya utumishi wa umma

Pia kushindwa kuzuia ujenzi wa holela katika maeneo yasiyo rasmi pamoja na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya ofisi hizo.
Chanzo -GPL
Comments
Post a Comment