Kocha mkuu wa Simba sc, Mcroatia, Zdravko Logarusic (wa kwanza kushoto) HAKUNA uchawi katika soka!. Kabumbu ni mipango na kupita njia sahihi ili kufikia kiwango cha juu. Tanzania ni miongoni mwa nchi `tia maji tia maji` kwenye mipango ya soka. Viongozi na mashabiki wanataka kupita njia ya mkato `short cut` ili kupata mafanikio. Moja ya kosa kubwa wafanyalo watu wengi ni kulifananisha soka letu na mataifa yaliyoendelea (barani Ulaya na Amerika). Utasikia mbona hata Chelsea, Man United, Barcelona wanafukuza makocha?, wanaacha wachezaji?. Kumbe klabu hizi zina mipango na zimekamatwa na wafanyabiashara ambao wamewekeza pesa zao. Hakuna mfanya biashara atayevulimilia hasara. Mtu anainunua klabu kwa mabilioni ya fedha, mfano Roman Abramovich wa Chelsea. Hawezi kuona kocha anavurunda na kumuacha, lazima achukue hatua kwasababu anataka faida. Pia klabu za Ulaya, mara nyingi kazi ya kocha ni kutengeneza timu kiuchezaji, (ufundi na mbinu za mpira). kwa asilimia