Abiria wote wa ndege ya Air Algerie waliangamia jangwani
Abiria wote na wahudumu wa ndege ya Air Algerie AH5017 waliangamia
jangwani.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi ya ufaransa
yamefaulu kupata mabaki ya ndege lakini hawakuweza kuokoa nafsi hata
moja.
Aidha rais Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi hao wamepata
mtambo wa kunukuu sauti ''Blackbox'' huko Mali ilikoanguka ndege hiyo
iliyokuwa ikielekea mji mkuu wa Algeria Algiers.
Abiria wote wa ndege ya Air Algerie waliangamia jangwani
Ndege hiyo ilikuwa imetoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou ikiwa na
Abiria 110 na wahudumu 6 .
Abiria 51 waliokuwa ndani ya ndege hii walikuwa ni raiya wa Ufaransa.
Wengine walikuwa 27kutoka Burkina Faso, 8 kutoka Lebanon , 6 kutoka
Algeria , 2 kutoka Luxembourg, 5 kutoka Canada, Wajerumani 4 .
Jamaa ya wahasiriwa wanakutana huko Ougadougu Burkina Faso
Abiria wengine walikuwa mmoja kutoka mataifa ya Cameroon , Ubeljiji ,Misri
Ukraine Uswisi Mnigeria na mmoja kutoka Mali.
Waziri wa Usalama wa ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve alisema ndege
hiyo iliyokuwa ikielekea Algiers kutoka mji mkuu wa Burkina Faso ,
Ougadougou,ilianguka kutokana na hali mbaya ya anga.
Comments
Post a Comment