Skip to main content

Posts

Showing posts from February 24, 2013

TUACHE SIASA KWENYE ELIMU YA TANZANIA! HABARI ZAIDI BOFYA HAPAA

             BY: MWANANCHI MWENYE UCHUNGU NA ELIMU YA TANZANIA SERIKALI MNAWADHARAU WANANCHI KWA KIGEZO CHA KWAMBA HAWAWEZI KUSEMA AU KUFANYA LOLOTE NDIO MAANA MNAAMUA KUWAFELISHA WANAFUNZI WA FORM FOUR WATOTO WA WALALAHOI KWA KUWA MNAJUA WATOTO WENU HAWATADHURIKA NA HILI, MNAANDAA TAIFA GANI SERIKALI YANGU MNAOJIITA SIKIVU? WAZIRI WA ELIMU PIA UMEKOSEA SANA KWA KUSEMA MTAWAPA WANAFUNZI HAO NAFASI NYINGINE YA KUFANYA MTIHANI,HII SIO HOJA THABITI KWANI ISSUE SIO KUFANYA MITIHANI ISSUE NI KWANINI WAFELI KWA NAMNA HIYO. SASA IMERIPOTIWA KUWA TUME IMEUNDWA NA WAZIRI MKUU KUCHUNGUZA CHANZO CHA MATOKEO MABAYA,JE TUME ITABADILISHA MATOKEO WAZIRI WANGU MKUU?JE HIZI ZERO AMBAZO NYINGI SIO ZA KWELI SITAISHA LINI?NAOMBA KWANZA MTENGANISHE SIASA NA TAALUMA KWANI HAVIENDANI HATA KIDOGO NI KAMA MAJI NA MAFUTA. NAOMBA PIA USAHIHISHAJI WA MITIHANI IANGALIWE UPYA,PIA JARIBUNI KUANGALIA MITAALA YA ELIMU ,VITABU PIA VIMEKUWA VINGI SANA ,JARIBUNI KUONA JE VITABU GANI VINAENDANA NA MITAALA YA ELIMU

TIMBULO NA ROSE NDAUKA KWENYE FILAMU MMOJA! JE NIFILAMU GANII BOFYA HAPAAAA

BAADHI YA CLIP YA UTENGENEZAJI WA FILAMU YA "WORLD FOR BENEFIT"ROSE NDAUKA NA TIMBULO WA KESHO  Rose na Timbulo kazini ROSE NDAUKA AKIWA KWENYE POZI Hapa maelekezo mawili matatu yakitoa  Bwana Timbulo katika shot 

IMAMU AUAWA KIKATILI HABARI ZAIDI BOFYA HAPA.....

                          Imamu wa Msikiti wa Mwakaje Zanzibar auawa                                                              SIKU chache baada ya kutokea kifo cha Padri Evarist Gabriel Mushi na watu wasiojulikana kwa kupigwa risasi kichwani eneo la Beit el Raas, Jana Imamu wa Msikiti wa Mwakaje amefariki dunia baada ya kupigwa mapanga hadi kufa. Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ahmada Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hapo jana mchana majira ya saa 8 mchana na kumtaja aliyefariki ni Sheikh Ali Khamis ambaye ameuawa na watu wasiojulikana. Kamanda Ahmada alisema Sheikh Khamis mbali ya kuwa ni Imamu wa Msikiti lakini pia ni mkulima na ameuliwa wakati akiwa katika mazingira ya kazi zake ndani ya shamba lake huko Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja. Akielezea mazingira ya tukio hilo Kamanda Ahmada alisema tukio hilo limetokea baada ya Sheikh Khamis kwenda shambani kwake katika shmba la minazi Kidoti ambapo wakati akiwa shamban