Skip to main content

Posts

Showing posts from June 22, 2014

MBASHA, FLORA WAPATANA, SABABU ZILIZOSABABISHA WAPATANE SOMA HAPA

Stori: WAANDISHI WETU HAKUNA neno zuri la kusema zaidi ya Mungu mkubwa! Ule mtafaruku ndani ya ndoa ya mwimba Injili mahiri Bongo, Flora na mumewe, Emmanuel Mbasha umedaiwa kumalizika kwa wawili hao kupatana, Risasi Jumamosi linakuwa nambari wani kukuhabarisha. Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, wawili hao walikalishwa kikao cha upatanishi mapema wiki hii kilichokuwa chini ya familia. Mume wa Flora Mbasha, Bw. Emmanuel Mbasha. MANENO YA CHANZO “Kikao cha familia kilikaa, Mbasha aliitwa akafika, Flora naye aliitwa akatokea, mazungumzo yalikuwa marefu lakini kimsingi waliamua kuweka kando mtafaruku wao na kuijenga upya ndoa yao,” kilisema chanzo. Chanzo kiliongeza kuwa katika kikao hicho cha mwanzoni mwa wiki hii, miongoni mwa adidu za rejea ilikuwa kutokumbushia vikao vilivyopita ambapo hakukupatikana muafaka. VIKAO VILIVYOPITA Katika vikao vilivyopita, wahusika wakuu walikuwa wazazi wa Mbasha (mzee Maneno Mbasha, Zulfa Maneno), ndugu wa Flora na Mchungaji wa Kani

RAIS KIKWETE AONGOZA MKUTANO WA KAMATI YA VIONGOZI WA AFRIKA KUHUSU TABIA NCHI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Kuhusu Tabia Nchi  ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon pembeni mwa mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika mjini Malabo, Equatorial Guinea leo Juni 27, 2014   PICHA NA IKULU

SERIKALI YATOA UFAFANUZI TAARIFA ZA MAGAZETI JUU YA HOTUBA YA KATIBU MKUU KIONGOZI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Katika baadhi ya magazeti ya leo tarehe 27 Juni, 2014 yameandika taarifa ambazo sio sahihi likiwemo gazeti la  Uhuru lenye kichwa cha habari “BILA KUPITIA JKT HAKUNA AJIRA SERIKALINI na gazeti la Tanzania Daima lenye kichwa cha habari “IKULU: RUSHWA YA NGONO IMEKITHIRI SERIKALINI”. Magazeti yote haya yameandika habari za kupotosha Umma kuhusu hotuba ya Katibu Mkuu Kiongozi aliyoitoa tarehe 26/6/2014 katika mkutano wa Mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Makatibu Tawala uliofanyika mjini Dodoma. Magazeti hayo yamejenga taswira kwamba Katibu Mkuu Kiongozi alitoa taarifa kwamba “Hakuna ajira bila kupitia Jeshi la Kujenga Taifa” na “Rushwa ya ngono imekithiri Serikalini”. Serikali inapenda kutoa ufafanuzi kwamba taarifa hizo siyo za kweli wala hazielezi taarifa halisi aliyoigusia Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Ombeni Sefue. Katika hotuba y

RASMI! MAHAKAMA YARUHUSU UCHAGUZI SIMBA SC KUFANYIKA JUNI 29

Mahakama yaruhusu uchaguzi ya Simba kufanyika juni 29 mwaka huu.  Na Baraka Mpenja, Dar es salaam   BAADA ya mizengwe kugubika uchaguzi wa Simba sc , sasa kimeeleweka baada ya mahakamu kuu kuruhusu mchakato huo kuendelea kama kawaida. Baadhi ya wanachama wa Simba walienda mahakama kuu wakihitaji chombo hicho cha dola kusimamisha uchaguzi wa Simba unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu. Sababu ya wanachama hao ilikuwa ni kupinga maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba, chini ya mwenyekiti wake, Wakili Damas Daniel Ndumbaro, kuliengua jina la aliyekuwa mgombe wa Urais, Michael Wambura kwa mara ya pili. Hii hapa ni kauli ya katibu mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga aliyotoa jioni hii

LUKE SHAW ASAINI MIAKA MINNE OLD TRAFFORD, ROONEY AMKARIBISHA KIROHO SAFI

Luke Shaw amekamilisha dili la usajili la paundi milioni 31.5 katika klabu ya Manchester United.  BEKI wa kushoto wa England, Luke Shaw amekamilisha usajili katika klabu ya Manchester United kwa dau la paundi milioni 31.5 na kusaini mkataba wa miaka minne kukipiga Old Trafford. Nyota huyo kinda amefuzu vipimo vya afya leo katika uwanja wa mazoezi wa Carrington na imetaarifiwa kuwa atakuwa chaguo la kwanza la kocha Louis van Gaal katika nafasi ya kushoto. Inafahamika kuwa kinda huyo atahakikishiwa nafasi ya kuanza, huku beki mkongwe mwenye miaka 33, Mfaransa, Patrice Evra ambaye atabakia kwa mwaka mmoja akipunguziwa majukumu. Historia: Shaw alisema amejisikia furaha kujiunga na mabingwa mara 13 wa ligi kuu ya England

COUTINHO AWASILI NA KUSEMA AMEKUJA KUISAIDIA YANGA SC

                                            Afisa Haari wa Young Africans Bw Baraka Kizuguto (kushoto) akiwa pamoja na mshambuliaji mpya Andrey Coutinho mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa JK Nyerer leo   Kiungo mshambuliaji mpya wa timu ya Young Africans SC  Andrey Marcel Ferreira Coutinho amewasili mchana wa leo jijini Dar es salaam akitokea kwao nchini Brazil tayari kabisa kwa kuanza kazi ya kuwatumikia wana Wanajangwani katika msimu wa 2014/2015.   Countinho amewasili mchana kwa shirika la Ndege la Afrika Kusini (South African Airways) akitoka jijini Sao Paul ambapo safari ya kuja Tanzania imemkchukua takribani masaa 20 tokea katika Mji wa Berem ambapo ndipo anapoishi. Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege  wa JK Nyerere, Coutinho alipokelewa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bw. Mohamed Bhinda ambaye alimuongoza kuwasilimia washabiki na waaandishi wa habari walijitokeza kumlaki.

MAXIMO ASAINI MIAKA MIWILI YANGA SC, KUANZA KUPIGA MZIGO JUMATATU

                                          Kocha Mkuu mpya wa Yanga SC Marcio Maximo (kushoto) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, kulia ni msaidizi wake Leonado Neiva  Kocha mbrazil Marcio Maximo leo amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuwatumikia Mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu ya Vodacom timu ya Young Africans pamoja na msaidizi wake Leonadro Neiva ambao wamesema wamekuja kuisaidia Yanga iweze kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali. Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, Maximo amesema anajiskia furaha sana kurudi kufanya kazi Tanzania, kwani watu wake ni wakarimu, wapenda mpira hivyo anaona kama yupo nyumbani japo awamu hii ni kwa majukumu ya ngazi ya klabu tofauti na awali alipokua ngazi ya Taifa

NIGERIA WAANZA `MIZINGUO` KOMBE LA DUNIA, WASUSIA MAZOEZI KISA POSHO!

Kikosi cha Nigeria katika kombe la dunia kimesusia kikao cha mazoezi kama ilivyopangwa kwa sababu ya kukosa kulipwa fedha zao za ziada.   Kitengo cha michezo cha BBC kimeelezwa kuwa wachezaji hao wanaamini kuwa wamelipwa kiasi cha dola 15,000 (pauni 8,800), chini ya pesa wanazopaswa kulipwa baada ya kufika katika mkondo wa pili wa kombe la dunia, huko Brazil.   Wachezaji hao wamesusia mazoezi katika uwanja wa Campinas na baadaye maafisa wakadai kwamba mazoezi hayo yalikuwa yametupiliwa mbali.   Nigeria inachuana na Ufaransa katika mechi ya muondowano siku ya Jumatatu baada ya kuchukua nafasi ya pili katika kundi lao la F.   Shirika la habari la BBC michezo limeelezwa kuwa shida imetokea katika ufafanuzi wa njia itakayotumika kuwalipa wachezaji hao pesa hizo za ziada. Wachezaji wa Nigeria wakimkaba mchezaji wa timu ya Argentina   Wachezaji hao wanaamini kuwa watapokea dola 10,000 kwa ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Bosnia-Hercegovina na dola 5,00

MTEMVU: WAPINZANI HATA WAKIUNGANA VIPI CCM ITAWABWAGA, ASHANGAA KUAMBIWA ANA MASLAHI BINAFSI KUWATETEA MAMALISHE

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya ya Temeke, leo katika ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo jijini Dar es Salaam. Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, akimkabidhi hati ya pongezi , Zaitun Lukinga, ya kuwa kiongozi wa Jumuia ya Wazazi awamu zaidi ya moja katika nafasi ya Katibu wa Jumuia ya wazazi Kata ya Kurasini, wakati wa mkutano huo leo  Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo. Habari Picha na Bashir Nkoromo- theNkoromo Blog NA BASHIR NKOROMO, TEMEKE MBUNGE wa Temeke Abbas Mtemvu amewananga wapinzani akisema hata wakisimamisha mgombea mmoja mmoja, katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, CCM itawabwaga. Amesema, uhakika huo anao na hata wapinzani wenyewe wanajua hilo, kwa kuwa hawaizidi CCM kwa weledi wa kisiasa, kwa akili wala wingi wa wanachama. Mtemvu amsema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Temeke, kilichofanyika leo, Juni 27, 2014, kwen