Kikosi cha Nigeria katika kombe
la dunia kimesusia kikao cha mazoezi kama ilivyopangwa kwa sababu ya
kukosa kulipwa fedha zao za ziada.
Kitengo cha michezo cha BBC
kimeelezwa kuwa wachezaji hao wanaamini kuwa wamelipwa kiasi cha dola
15,000 (pauni 8,800), chini ya pesa wanazopaswa kulipwa baada ya kufika
katika mkondo wa pili wa kombe la dunia, huko Brazil.
Wachezaji hao wamesusia mazoezi katika uwanja wa Campinas
na baadaye maafisa wakadai kwamba mazoezi hayo yalikuwa yametupiliwa
mbali.
Nigeria inachuana na Ufaransa
katika mechi ya muondowano siku ya Jumatatu baada ya kuchukua nafasi ya
pili katika kundi lao la F.
Shirika la habari la BBC michezo
limeelezwa kuwa shida imetokea katika ufafanuzi wa njia itakayotumika
kuwalipa wachezaji hao pesa hizo za ziada.
Wachezaji wa Nigeria wakimkaba mchezaji wa timu ya Argentina
Wachezaji hao wanaamini kuwa
watapokea dola 10,000 kwa ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Bosnia-Hercegovina
na dola 5,000 kwa sare yao dhidi ya Iran.
Comments
Post a Comment