Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amesema kuwa, Serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara ili wawekezaji wa nje na ndani waweze kutekeleza majukumu yao bila kikwazo. Dk Kigoda aliyasema hayo juzi usiku alipokuwa kwenye hafla ya kuzitambua Kampuni 100 Bora zinazokua kwa kasi nchini (Top 100 Mid–Sized Companies), ambapo Kampuni ya Kipipa Millers Limited ya jijini Mwanza ilishika nafasi ya kwanza. Kampuni hizo zilitambuliwa na kupewa tuzo kutokana na shindano linaloendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) na KPMG Tanzania na kudhaminiwa na Benki ya NBC pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Dk Kigoda alisema shindano hilo linaimarika kila mwaka na lina nafasi kubwa ya kuimarisha uchumi kwa Kampuni za Afrika Mashariki. Alisema ili kampuni hizo ziweze kufikia mafanikio, Serikali itajitahidi kuweka mazingira yatakayoziwezesha kufanya shughuli zake vizuri na kufanya uzalishaji kwa gharama n