KILI STARS YAIKOMALIA ZAMBIA MICHUANO YA CECAFA, YATOKA SARE YA 1-1, BURUNDI YAWAADHIBU MABAHARIA WA SOMALIA!!
TIMU
ya Taifa ya Tanzania bara, The Kilimanjaro Stars imeanza kwa sare
michuano ya Mataifa ya Afrika mashariki na kati, CECAFA Challenge baada
ya jioni ya leo kufungana bao 1-1 na waliowahi kuwa mabingwa wa Afrika,
timu ya Taifa ya Zambia maarufu kwa jina la Chipolopopo kwenye uwanja wa
Kenyatta, Machakos, Kenya.
Zambia
walikuwa wa kwanza kuandika bao katiKa mchezo huo wa kundi B kupitia
kwa nyota wake Ronald Kampamba dakika ya 41, akiunganishwa kwa kichwa
`ndosi` krosi iliyochongwa na aliyewahi kuwa mchezaji bora wa Afrika wa
Tuzo ya BBC, Felix Katongo.
Chipolopolo
walitawala zaidi mchezo huo kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi
nyingi za kupata magoli, lakini umahiri wa kipa mkongwe Ivon Philip
Mapunda uliiokoa stars kwani aliokoa michomo kadhaa ya Wazee wa Risasi
za Shaba.
Kipindi
cha pili, Kili Stars ilicheza mpira mzuri na katika dakika ya 48
walipata bao kupitia kwa beki Said Morad akiunganisha mpira wa kona
uliochongwa na kiungo mahiri Salum Abubakar ‘Sure Boy’ .
Bao
hilo liliwapa nguvu Stars na kuanza kusaka soka la uhakika na kuwaacha
Zambia wakihaha huku na kule, lakini mlinda mlango wao, Nsabata Toaster
aliwasaidia sana kwa kuokoa hatari nyingi langoni mwake.
Kikosi
cha Stars kilikuwa; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad,
Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Ramadhani Singano
‘Messi’ dk89, Hassan Dilunga/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk85, Elias
Maguri/Haroun Chanongo dk72, Amri Kiemba na Mrisho Ngassa.
Chipolopolo;
Nsabata Toaster, Bronson Chama, Jimmy Chisenga/Kabaso Chongo dk67,
Christopher Munthali, Rodrcik Kabwe, Stanley Nshimbi/Alex Nshimbi dk57,
Sydney Kalume, Kondwani Mtonga, Felix Katongo/Salulani Phiri dk73,
Ronald Kampamba na Festus Ndewe.
Mchezo
wa mapema uliwakutanisha timu ya Taifa ya Burundi dhidi ya Somalia na
kushuhudia Warundi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye uwanja wa
Kenyatta, Machakos nchini Kenya.
Mabao ya Burundi yalitiwa kambani na nyota wake Abdoul Fiston dakika ya 40 na Nduwarugira Christopher dakika ya 55.
Kwa
matokeo ya mechi za leo za kundi B, Burundi wanaongoza kundi hilo kwa
pointi tatu wakifuatiwa na Kili Stars na Zambia wenye pointi moja, huku
wasomali wakiburuza mkia.
Comments
Post a Comment