Skip to main content

Posts

Showing posts from June 1, 2014

JACOB ZUMA ALAZWA

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amelazwa hospitalini kwa uchunguzi wa afya atapumzika kwa muda ingawa ataendelea na majukumu akiwa nyumbani Taarifa hii ni kwa mujibu wa maafisa kutoka kwa ofisi yake. Taarifa hiyo ilisema kuwa Zuma atalazimika kumpumzika kwa muda ingawa ataendelea na majukumu yake ya kitaifa akiwa nyumbani.  “Hapo jana Ijumaa Rais Zuma alishauriwa kupumzika hasa baada ya msimu wa uchaguzi kukamilika wiki chache zilizopita. Madaktari hawajaeleza wasiwasi wowote kuhusu afya yake". CHANZO BBC SWAHILI

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MWANDAMIZI WA MAMBO YA NDANI NA NJE WA SINGAPORE

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo  na  Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli, Ikulu jijini Dar es salaam Mei 6, 2014. Waziri huyo na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano. PICHA NA IKULU Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo  na  Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli, Ikulu jijini Dar es salaam Mei 6, 2014. Waziri huyo na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na   Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli, na ujumbe wake  Ikulu jijini Dar es salaam Mei 6, 2014. Waziri huyo  yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Wa pili kutoka kulia mstari wa mbele ni  Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu

MARCO REUS APATA MAJERUHI MBAYA UJERUMANI IKISHINDA 6-1, HATARINI KUZIKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA

 Hoi : Kiungo wa Ujerumani,  Marco Reus akiwa ameshika kifundo chake cha mguu wa kushoto baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Armenia    Reus akitibiwa na madaktariwa timu ya taifa ya Ujerumani.  PIGO!,  Marco Reus hatihati kucheza fainali za kombe la dunia baada ya jana kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika ushindi wa mabao 6-1 ambao Ujerumani ilivuna dhidi ya Armenia ikiwa ni pasha pasha kabla ya kuanza  kombe la dunia wiki ijayo. Nyota huyo Borussia Dortmund alianguka chini baada ya kugongana na kiungo wa Armenia, Artur Yedigaryan na kuambulia kuumia na kuzua hofu kubwa kwa mashabiki wa Ujerumani na benchi zima la ufundi.

BRAZIL 1 vs 0 SERBIA: FRED AWAOKOA, LAKINI MASHABIKI WAZOMEA KIWANGO `MBOFU MBOFU` YA SAMBA

Aliwaokoa: Fred aliifungia bao pekee Brazil katika pasha pasha ya kombe la dunia. Fred akichukua mpira katika dakika ya 58 na kufunga bao kwenye uwanja wa  Morumbi WAZEE wa Samba, Brazil,  jana usiku walibanwa mbavu na kuanza vibaya kipindi cha kwanza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Serbia na kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 wakati huu zikisalia zimesalia siku tano tu kuanza fainali za kombe la dunia. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mashabiki waliofurika uwanjani waliwazomea wachezaji wa Brazil baada ya Fred kufunga bao hilo pekee katika dakika ya 58. Kusoma zaidi bofya

SCOLARI: KUZOMEWA SIO TATIZO KWA BRAZIL

KOCHA Luiz Felipe Scolari amesema kitendo cha mashabiki kuwazomea wachezaji wa tiimu ya Taifa ya Brazil katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Serbia jana ijumaa haina tatizo kwake na kwa wachezaji wake kwani wapo tayari kwa mazingira kama hayo.  Selecao walihangaika kuvunja ngome imara ya Serbia katika dimba la Sao Paulo mpaka Fred alipofanikiwa kupenya katika dakika ya 58 na kufunga bao hilo pekee.  Mashabiki walikosa uvumilivu na kujikuta wakiwazomea wachezaji wao kwa soka `mbofu mbofu` dhidi ya Serbia, lakini Scolari hana tatizo na kitendo hicho. “Ni kitu cha kawaida,” Kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari wa Brazil. “Ilitokea Goiania na sehemu nyingine”.  “Haikuwa tatizo kwa mchezaji wangu yeyote. Wako tayari kwa hili”.  “Lakini baada ya filimbi ya mwisho, asilimia 65 ya mashabiki 67,000 waliridhishwa”.

RAMBIRAMBI MSIBA WA KANALI MWANAKATWE

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wake (wakati huo ikiitwa FAT), Kanali mstaa fu Ali Hassan Mwanakatwe kilichotokea leo asubuhi (Juni 7 mwaka huu) katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa binti wa marehemu, Sophia, baba yake alianguka bafuni nyumbani kwake Mbezi Beach ambapo alikimbizwa katika Hospitali ya Lugalo ambapo ndipo umauti ulipomfika wakati madaktari wakimpatia matibabu. Kanali Mwanakatwe alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) katika uchaguzi uliofanyika mwaka 1993 mjini Kibaha mkoani Pwani. Baada ya kuondoka FAT, aligombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kufanikiwa kushinda katika uchaguzi uliofanyika mwaka 1997. Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini na Afrika kwa ujumla kwani, Kanali M

ZIARA YA WAZIRI MKUU PINDA WILAYANI CHAMWINO DODOMA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bibi  Gilita  Mlong’ose  wakati alipotembelea  Hospitali ya Mvumi wilayani Chamwino akiwa katika ziara ya wilaya hiyo mkoani Dodoma Juni 7, 2014. Bibi huyo alikuwa ni miongoni mwa wagonjwa walipfika  hospitalini hapo kutibiwa macho. Kushoto ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde. (Picha na Ofisiya Waziri Mkuu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bibi  Gilita  Mlong’ose  wakati alipotembelea  Hospitali ya Mvumi wilayani Chamwino akiwa katika ziara ya wilaya hiyo mkoani Dodoma Juni 7, 2014. Bibi huyo alikuwa ni miongoni mwa wagonjwa walipfika  hospitalini hapo kutibiwa macho. Kushoto ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde. (Picha na Ofisiya Waziri Mkuu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi ya mkuki kutoka kutoka kwa mwenyekiti waCCM wa Tawi la  Ilolo wilayani Chamwino akiwa katika ziara  ya wilaya hiyo mkoani Dodoma Juni 7, 2014. Katikati  ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wizara ya uchukuzi yaadhimisha wiki ya mazingira duniani kwa kupanda miti bandarini

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wizara ya Uchukuzi, Bw. Issa Nchasi, akifanya usafi katika eneo la bandari ya Dar es Salaam kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Tunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Tanzania’. Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake wakiwa kwenye zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingiza Duniani. Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi, Bi, Tumpe Mwaijande (kulia), akipanda mti katika eneo la bandari ya Dar es Salaam leo asubuhi, kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira. Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira yanafanyika kitaifa mkoani Mwanza ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Tunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Tanzania’. (Picha na kitengo cha mawasiliano Serikalini-Uchukuzi

HII NDIO TAARIFA KAMILI JUU YA JOKA LA AJABU LILILOKUWA LIKIFUGWA NA MTU ANAYESADIKIWA NI MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA

JOKA KUBWA LAUWAWA ARUSHA Na Victor Amath Joka kubwa aina ya Chatu ameuawa jana na Wananchi wenye hasira kali mtaa wa Azimio kata ya Kiranyi jijini  Arusha baada ya kuonekana nyumbani kwa mtu anayefahamika kwa jina  la Joseph Magesa . Aidha tukio hilo la kusimimua la la aina yake lilitokea jana majira ya saa 4 asubuhi ambapo inaelezwa kuwa joka huyo alipasua kioo cha nyumba na kutoka nje hali iliyompelekea mototo wa Magesa kuimbia nyumba hiyo pamoja na mlinzi. Baada ya Wananchi kupata taarifa za kuonekana kwa joka hilo nyumbani kwa magesa  walifika nyumbani hapo na kumkuta nyoka huyo mkubwa akiwa anataambaa kuelekea nje ya geti ndipo alipojitokeza kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja na kumvuta nyoka huyo kwa kutumia vitambaa alivyokuwa amefungiwa kwenye mkia. George Enock ni mkazi wa eneo hilo ameeleza kuwa baada ya nyoka huyo kukamatwa alitembezwa mtaani mpaka majira ya saa 7 mchana ambapo alikatwa katwa na mapanga vipande baada ya hapo akateketezwa kwa moto. Mkazi

NDOA YA FLORA MBASHA CHALI..FLORA AHAMIA KWA GWAJIMA, PRADO LADAIWA KUWA NI CHANZO

BAADA ya kudumu kwa zaidi ya miaka 10, imebainika kuwa ndoa ya mwanamuziki mahiri wa muziki wa Injili Bongo, Flora na mumewe Emmanuel Mbasha ipo chali kwa maana ya kuanguka huku ikidaiwa kuwa, kusimama imara tena inawezekana lakini ni kazi kubwa, Amani limefukunyua mazito Hilo limejitokeza wiki moja baada ya madai ya mwanaume huyo kudaiwa kumbaka shemeji yake na kesi ipo polisi. Imeelezwa Flora na mumewe ambao walifunga ndoa Agosti 22, 2002 wamepita katika migogoro mizito lakini wawili hao walikuwa wakiyamaliza kifamilia hadi kufikia hili la hivi karibuni ndilo lililoziba mataumaini ya wawili hao kuishi kama mume na mke. Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimeeleza kuwa, mzizi wa wawili hao kugombana ulichochewa na mwanamke mmoja (jina tunalo) ambaye alikuwa akikinzana na ushauri wa Mbasha mara kwa mara. “Kuna vitu Mbasha alikuwa akimshauri huyo mama lakini walikuwa wakipishana Kiswahili  na hapo ndipo tatizo lilipokua hadi kufikia hatua ya kumwagan