Skip to main content

Posts

Showing posts from March 17, 2013

Tajiri wa Urusi afariki! habari zaidi bofyaa hapa...

    Kilichosababisha kifo cha tajiri Boris Berezovsky, mwenye umri wa miaka 67, bado hakijajulikana. Polisi bado wanachunguza kilichosababisha kifo cha Berezovsky Kilichosababisha kifo cha tajiri Boris Berezovsky, mwenye umri wa miaka 67, bado hakijajulikana. Tajiri huyo alikuwa akisakwa mno nchini Urusi, na anafahamika kuwa mpinzani mkali wa Rais Zamani alikuwa na mamlaka na ushawishi sana katika bunge la Kremlin, lakini yote hayo yalididimia mara tu alipoingia Bw Putin, na Berezovsky alikimbilia Uingereza kuanza maisha ya uhamishoni mwaka 2000. Awali idara ya polisi ya Thames Valley ilitangaza kwamba ilikuwa katika hatua za kuchunguza kifo cha mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 67, katika eneo la Ascot, Berkshire. (maelezo zaidi baada ya muda mfupi)

JEFFREY MATHEBULA NA TALAKALANI NDLOVU WACHAPANA LEO! BOFYA KWA UNDANI ZAIDII

JEFFREY MATHEBULA NA TAKALANI NDLOVU KUWANIA UBINGWA WA DUNIA     Mabondia wa Afrika ya Kusini Jeffrey Mathebula na Takalani Ndlovu watakutana katika ukumbi wa Carnival City Casino jijini Johannesburg jimbo la Gauteng nchini Afrika ya Kusini katika pambano la mchujo (Elimination Title) la ubingwa wa dunia uzito wa unyoya (Featherweight). Wawili hawa ni mahasimu wakubwa wanaojulikana nchini Afrika ya Kusini na walishakutana mara mbili ambapo Ndlovu alishhinda pambano la awali huku Mathebula akishinda pambano la mwisho. Wakati huo huo mabondia Vusi Malinga wa Afrika ya Kusini na Diarh Gabutan wa Phillipines watakutana katika mpambano mwingine wa mchujo kuwania tiketi ya kukutana na bingwa wa dunia katika uzito wa Bantam. Promota maarufu wa Afrika ya Kusini Branco Milenkovic wa kampuni ya Branco Boxing Promitions atakuwa ndiye mwandaaji wa mpambano huo utakaofanyika tarehe 23 mwezi wa tatu mwaka huu. Huu ni mwendelezo wa Shirikisho la Ngumi la kKmataifa IBF katika pro

TANZANIA YASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIDHAA ZA CHAKULA DUNIANI! BOFYA HAPA KWA UNDANI ZAIDIII

USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIDHAA ZA CHAKULA DUNIANI YANAYO ANZA LEO TAREHE 17 /03/ 2013 KWENYE UKUMBI WA MAONYESHO WA EXCEL, LONDON   HABARI ZA LEO NDUGU ZANGU, MATUMAINI YETU KWA UWEZO WA MWENYEZI MUNGU NYOTE MPO SALAMA KABISA. KUTOKA UBALOZI WA TANZANIA HAPA NCHINI UINGEREZA, TUNA TAARIFA NDOGO YA KUSHARE NA WATANZANIA WOTE. KITUO CHA BIASHARA, LONDON (TANZANIA TRADE CENTRE) KINAPENDA KUWAFAHAMISHA WATANZANIA WAISHIO NCHINI UINGEREZA, KUWEZA KUFIKA KATIKA JUMBA LA MAONYESHO LA EXCEL CENTRE, LONDON, KWENYE MAONYESHO MAKUBWA YA KIMATAIFA YA BIDHAA ZA CHAKULA, MAONYESHO HAYO YAJULIKANAYO KAMA INTERNATIONAL FOOD FESTIVAL (IFE 2013). KWENYE MAONYESHO HAYO, MAKAMPUNI YAPATAYO SITA (6), YANAIWAKIRISHA NCHI YETU TANZANIA. BIDHAA ZINAZO ONYESHWA NA MAKAMPUNI KUTOKA TANZANIA NI:- CHAI, KAHAWA, VIUNGO MBALIMBALI VYA CHAKULA, MAFUTA YA KUPIKIA, MVINYO (WINE) ZA AINA MBALIMBALI. MADHUMUNI MAKUBWA YA MAONYESHO HAYO KWA UPANDE WA TANZANIA, NI KUTANGAZA

MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUWA MTANGAZAJI MZURII! KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPAA

MATAMSHI NI LAZIMA KUZINGATIA KATIKA UTANGAZAJI! MWANDISHI WA HABARI NA MTANGAZAJI AMANI JAMES Hili ni muhimu kabisa katika kazi ya utangazaji. Hapa tunazungumzia unavyoweza kutamka kwa ufasaha maneno hasa ikizingatiwa BBC inaaminika na wasikilizaji wake tangu zamani kuwa ina weledi wa lugha ya Kiswahili. Haipendezi na utaonekana kichekesho ukichanganya L na R na hili la siku hizi linalowapa taabu kubwa vijana la H na A. Ama watu nane badala ya watu wanane. Ni nzuri na si nzuli, habari na si abari. Wapo wanaotamka mathalan watu nane wameuawa .....Kiswahili hakikubali hilo, bali unachotakiwa kutamka ama kuandika ni watu wanane. Jee ikiwa kwa idadi ya watu wawili ukikatisha kama ilivyo kwa nane utatamkaje? ni watu mbili! Hapana ni watu wawili. Neno jingine linalowasumbua waandishi kuliandika na kulitamka ni dharura, wapo wanaoliandika na kulitamka dharula ni makosa kutumia dharula ila ni dharura. Hili ni muhimu kabisa.

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO! HABARI ZAIDII BOFYA HAPAAAAAAAAAAA

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO . . . . . . . . . . . . .

KIJANA ALIYEANDAA VIDEO YA LWAKARE NAYE AMEKAMATWA

KIJANA ALIYEANDAA VIDEO YA LWAKARE NAYE AMEKAMATWA Anayedaiwa kupiga video iliyosababisha kukamatwa kwa Rwakatale ( pichani ) maarufu kwa jina la Ludovik Joseph amekamatwa mkoani Iringa . kijana huyo anadaiwa kuwa ni mhitimu wa chuo kikuu cha DUCE -------------------------------- Ndugu zangu, Usiku huu nikiwa kwenye shughuli ya shule ya watoto wangu pale Highlands Hall Iringa nilifikiwa na habari kuwa Kijana Ludovick amekamatwa na polisi kuhusiana na tuhuma za kuhusika na kuteswa mwandishi Absalom Kibanda. Namfahamu kijana Ludovik tangu akiwa Chuo Kikuu ( DUCE). Ni mmoja wa Watanzania wengi walionifahamu kupitia kazi zangu za magazetini. Kwangu Ludovick ni kijana mtaratibu na mpole sana, na hata niliposikia habari hizi kwa namna fulani nimeshtushwa nazo. Ludovick ambaye amekuwa akiishi Dar ni mmoja wa vijana waliokuwa wakinisaidia kwa kujitolea kwenye kazi zangu za mitandaoni, hususan kwenye Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii.