Skip to main content

Posts

Showing posts from May 25, 2014

TAZAMA JINSI MASTAA BONGO MUVI WALIVYOANGUA KILIO KUMLILIA RECHO

Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere akilia kwa uchungu. Huzuni tele ikiwa imetawala wasanii waliokuwa viwanja ya Leaders. Bi. Mwenda akilia kwa uchungu. Mume wa Rachel aitwaye Saguda akiwa na majonzi. Mwigizaji Johari akiwa na huzuni. Cathy Rupia  akiomboleza. Steve akizungumza na wanachama wa Bongo Muvi, viwanja vya Leaders. Bongo Muvi wakijadili cha kufanya. Wasanii wakipanga utaratibu wa msiba wa mwenzao. Wasanii wa Bongo Muvi wakiwa Muhimbili baada ya kupata habari za kifo cha mwenzao. MASTAA wa Bongo Muvi wamemlilia msanii mwenzao, Rachel Haule 'Recho' aliyefariki jana saa mbili usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar baada ya kujifungua ambapo mtoto wake alifariki muda mfupi na baadaye yeye akafariki. Kwa mujibu  wa mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve ‘Nyerere’, mwili wa Rachel utasafirishwa kwenda kwao Songea kwa ajili ya maziko.  Habari nyingine za msiba zitatolewa wakati wowote na mtandao huu mara tu zinapopatikana.

MUME NA MKE WANUSURIKA KUFA KWA KUUNGUA MOTO,TAZAMA PICHA ZINASIKITISHA

  Majeruhi bi Happiness Chacha (22) akiwa amelazwa katika wodi namba 8 katika hospitali ya wilaya ya Geita baada ya kuungua moto yeye na mme wake -Picha zote na Valence Robert Majeruhi Chacha Wambura (35)akiwa amelazwa katika wodi namba 7 katika wilaya ya Geita baada ya kuungua moto katika kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita mkoani Geita. Wanandoa wawili wakazi wa kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita mkoani Geita Happiness Chacha(22) na mme wake Chacha wambura(35) wamenusurika kufa baada ya nyumba yao kuungua moto katika kibanda chao cha bar. Tukio hilo limetokea jana usiku saa nane usiku katika kijiji cha Lwamgasa ambapo kufuatia tukio hilo majeruhi wakikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Geita mkoani Geita walipolazwa wodi namba 7 na 8. Robina Isack anayewauguza amesema kuwa usiku huo wa saa 8 waliona moto unawaka bila kujua umeanzia wapi huku wakishangaa kwa vile hawatumii nishati hiyo ya umeme na wala hapakuwa na moto waliokuwa wamewasha ndani. Kamanda wa polisi mkoa wa