Skip to main content

Posts

Showing posts from October 19, 2014

Waandamanaji,Serikali kukutana:Hong Kong

Hong Kong Wanafunzi wanaoongoza mgomo kwa zaidi ya wiki tatu Hong Kong leo wanatarajiwa kukutana na uongozi wa serikali kwa majadiliano zaidi kuhusiana na kumaliza mgomo. Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Hong Kong kuwa na mazungumzo rasmi na waandamanaji hao,na mkutano huo unatarajiwa kutangazwa moja kwa moja kupitia runinga. Hata hivyo kiongozi wa Polisi Hui Chun -Tak amewatahadharisha waandamanaji hao kusimama mbali na majengo ya serikali ya eneo la Mong Kok mahala ambapo pamekuwa kitovu cha mapambano kati ya polisi na waandamanaji hao katika siku za hivi karibuni. Vyombo vya habari vimesema kuwa hali katika mji wa Hong Kok ni mbaya na inaweza kusababisha machafuko na mapambano zaidi kama haidhibitiwa.

Mapigano yaanza tena Nigeria

Boko Haram Taarifa kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria zinasema zaidi ya watu ishirini wameuawa katika mapigano kati ya wanajeshi na wanamgambo wa kundi la Boko Haram, licha ya makubaliano ya kusitisha vita kufanyika ijumaa iliyopita. Vurugu zilifanyika siku ya katika mji wa Damboa. Makubaliano ya kusitisha vita kati ya wanamgambo wa Boko Haram na serikali ya Nigeria yanatarajiwa kuwaokoa wasichana zaidi ya mia mbili waliotekwa na kikundi hicho mwezi Aprili mwaka huu. Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema mapigano hayo yameleta hali ya wasiwasi kuhusiana na uwezekano kusitisha mapigano hayo.

Ebola na utaratibu mpya wa Mazishi

madaktari wa Ebola Ugonjwa wa Ebola unahitaji hatua za haraka na umakini katika kuhifadhi miili ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huo, hii ina maana kuwa hatua hiyo inaondokana na taratibu za kawaida zilizozoeleka za mazishi katika nchi zilizoathirika, ikiwemo matumizi ya mifuko mikubwa ya plastiki ambayo ni mbadala wa majeneza. Mabadiliko haya yanawaathiri wafanyabiashara wanaojipatia kipato kwa kutengeneza majeneza na wanaotoa huduma za mazishi Taarifa yake Mwandishi wa BBC mjini Monrovia nchini Liberia amebaini kuwa biashara hiyo imedorora. Wafanya biashara wa majeneza wanasema kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola wateja hawapatikani kwa wingi sababu ikielezwa kuwa watu waliopoteza maisha huhusishwa na maradhi ya ebola. Serikali ya Liberia imesema kuwa watu waliokufa hawatazikwa wakiwa ndani ya majeneza isipokuwa kwenye mifuko mikubwa ya Plastiki.

WAZIRI MKUU AALIKA WAWEKEZAJI KATIKA AFYA, KILIMO, NISHATI

*Obasanjo asisitiza ajira kwa vijana wa Afrika WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imefungua milango kwa wawekezaji kwenye sekta zote lakini mkazi unaelekezwa zaidi kwenye sekta ya afya, kilimo hasa usindikaji mazao, nishati na miundombinu. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Oktoba 20, 2014) wakati akishiriki Mjadala wa Marais (Presidential Keynote Panel) kuhusu fursa za uwekezaji barani Afrika uliolenga kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo barani Afrika hasa katika nchi za Tanzania, Uganda, Ghana na Rwanda ambao umeanza leo kwenye hoteli ya Savoy, jijini London, Uingereza. Waziri Mkuu aliwasili jijini London jana mchana kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi unaohusu uwekezaji barani Afrika (The Global African Investment Summit – TGAIS) kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete na ameshiriki mjadala huo pamoja na Rais John D. Mahama wa Ghana, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda. “Tunahitaji wawekezaji kwenye sekta nyingi lakini zaidi kwenye sekta ya af

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA WATAALAM WA HUDUMA ZA HABARI NA MAKTABA ZA AFYA AFRIKA (AHILA) JIJINI DAR ES SALAAM.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa 14 wa Wataalam wa Huduma za Habari na Maktaba za Afya Afrika (AHILA) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2014. Picha na OMR   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa 14 wa Wataalam wa Huduma za Habari na Maktaba za Afya Afrika (AHILA) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2014. Picha na OMR   Baadhi ya wadau wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akiwahutubia  alipokuwa akifungua rasmi Mkutano wa 14 wa Wataalam wa Huduma za Habari na Maktaba za Afya Afrika (AHILA) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 20, 2014. Picha na OMR Baadhi ya wadau wa mkutano huo wa