Hong Kong |
Wanafunzi wanaoongoza mgomo kwa zaidi ya wiki tatu Hong Kong leo wanatarajiwa kukutana na uongozi wa serikali kwa majadiliano zaidi kuhusiana na kumaliza mgomo.
Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Hong Kong kuwa na mazungumzo rasmi na waandamanaji hao,na mkutano huo unatarajiwa kutangazwa moja kwa moja kupitia runinga.
Hata hivyo kiongozi wa Polisi Hui Chun -Tak amewatahadharisha waandamanaji hao kusimama mbali na majengo ya serikali ya eneo la Mong Kok mahala ambapo pamekuwa kitovu cha mapambano kati ya polisi na waandamanaji hao katika siku za hivi karibuni.
Vyombo vya habari vimesema kuwa hali katika mji wa Hong Kok ni mbaya na inaweza kusababisha machafuko na mapambano zaidi kama haidhibitiwa.
Comments
Post a Comment