Skip to main content

Posts

Showing posts from August 24, 2014

Ugonjwa wa Ebola yaingia afrika mashariki kwa habari zaidi soma hapaa!!!

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imesema watu wawili wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola, uliolipuka kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo. Hao ni wagonjwa wa kwanza wa Ebola kuripotiwa nje ya Afrika Magharibi tangu kuzuka kwa ugonjwa huo huko, ingawaje haijaeleweka wazi kama vifo vya watu hao vinahusiana na mlipuko wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi. Mpaka sasa watu 1,427 wamekufa kutokana na maambukizo ya virusi vya Ebola. Shirika la Afya Duniani, WHO limesema kasi na kiwango cha milipuko hiyo hakijawahi kutokea hapo kabla. Watu wanaokadiriwa kufikia 2,615 Afrika Magharibi wameambukizwa ugonjwa wa Ebola tangu uzuke mwezi Machi mwaka huu. Kirusi cha Ebola Hakuna tiba inayojulikana kutibu ugonjwa huu lakini baadhi ya watu walioambukizwa virusi vya Ebola wamepata nafuu baada ya kupewa dawa ya Zmapp iliyo katika majaribio. Hata hivyo dawa hiyo imeadimika kwa sasa. Pia Jumapili, mfanyakazi wa afya wa Uingereza aliambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Sie