MARCO REUS APATA MAJERUHI MBAYA UJERUMANI IKISHINDA 6-1, HATARINI KUZIKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA


PIGO!, Marco Reus hatihati kucheza fainali za kombe la dunia
baada ya jana kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika ushindi wa
mabao 6-1 ambao Ujerumani ilivuna dhidi ya Armenia ikiwa ni pasha pasha
kabla ya kuanza kombe la dunia wiki ijayo.
Nyota huyo Borussia Dortmund
alianguka chini baada ya kugongana na kiungo wa Armenia, Artur
Yedigaryan na kuambulia kuumia na kuzua hofu kubwa kwa mashabiki wa
Ujerumani na benchi zima la ufundi.
Comments
Post a Comment