Watoto wakiwa mbele ya jengo lililoteketezwa Syria |
Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa vita nchini Syria vimesababisha kuharibu watoto kimwili na kisaikolojia.
Wakimbizi watoto walio katika umri wa kwenda
shule ambao wamekimbilia katika nchi jirani wameendelea kukosa elimu na
wanalazimika kufanyakazi ili kujikimu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi limesema watoto wapatao 300,000 wanaoishi nchini Lebanon na Jordan huenda wakakosa masomo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2013.
Wengi wa ambao hawaendi shuleni wanakwenda kufanyakazi kwa muda mrefu wakipata malipo kidogo, wakiwa na umri mdogo wa hata miaka saba.
Zaidi ya nusu ya wakimbizi wa Syria milioni 2.2 ni watoto, wengi wakikabiliwa na hatari kubwa na hata nje ya eneo la vita.
Hatari hizo ni pamoja na athari za kimwili na kisaikolojia.
Akizindua ripoti hiyo, Kamishina wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Antonio Guterres alisema: "Kama hatutachukua hatua haraka, kizazi cha watu wasio na hatia kitaishia kufa kutokana na vita."
Utafiti huu ni mpya kabisa na unajaribu kuonyesha madhara makubwa kwa watoto kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria vilivyodumu kwa miaka mitatu. Madhara hayo ni kwa watoto walio ndani na nje ya mipaka ya Syria.
Comments
Post a Comment