Timu ya soka ya Nigeria |
Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi ,
anasisitiza kuwa hana wasiwasi wowote kwamba anaweza kufutwa kazi kabla
ya kombe la dunia la Brazil la mwaka wa 2014.
Chini ya uongozi wa Keshi, Nigeria ilifanikiwa
kufika fainali ya mwaka ujao baada ya kushinda Ethiopia 4-1 katika mechi
za kufuzu kushiriki mchuano huo.Ingawa Keshi aliyekuwa nahodha wa hapo awali wa Super Eagels, amekosa mechi mara mbili baada ya kampeni ya timu hiyo kufuzu kwa michuano hio.
Mwaka wa 2002 Keshi alikua msaidizi wa Shuaibu Amodu wakati Nigeria ilifuzu kucheza kombe la dunia, lakini wawili hao walifutwa kazi na nafasi yao kuchukuliwa na Adegboye Onigbinde kabla ya mechi za mwisho zilizochezwa Korea Kusini na Japan.
Miaka minne baadaye Keshi pia alifutwa kazi na Togo kabla ya kombe la dunia la 2006 nchini Ujerumani, ingawa alikuwa ameiongoza timu kwa mara ya kwanza hadi sasa katika historia ya nchi hio.
Hivyo basi Keshi akawa na wasiwasi kua kilichotendeka hapo awali kingejirudia kwa mara nyingine, lakini Keshi mwenye umri wa miaka 51 ana mtizamo wake wa kipekee kuhusu hali ya mchezo wa kandanda.
"kazi hii ni ya kuajiri na kufuta," Keshi alilielezea BBC michezo. "nilipofutwa kazi mwaka wa 2002 nilipata mshtuko lakini hiyo ni hali ya maisha, kwa hivyo hatuwezi kujuta na kuishi kwa machungu na masikitiko.
"tunaongea kuhusu Nigeria kwa hivyo huwezi jua kitakacho tendeka.
"lakini cha muhimu sasa hivi ni kuwa tunatazamia tu yale yajayo ambayo ni kuandaa wachezaji wangu pekee.''
"huezi jisikitisha na yaliyofanyika ama yanayoweza fanyika. Tumefaulu zaidi ya matarajio ya watu kadhaa, zoezi la kujijenga linaendelea.
"siishi na hofu ya kufutwa kazi. Kwa kusema kweli hiyo ni kumaliza tu nguvu.
Keshi alikuwa na uhusiano mgumu na waajiri wake wa shirikisho la soka la Nigeria tangu kuongoza kikosi ambacho hakikuwa na ujuzi kushiriki na kushinda kombe la taifa bingwa Afrika, kwenye mchuano uliofanyika nchini Afrika Kusini mwanzoni mwa mwaka 2013
Comments
Post a Comment