
BEKI wa kushoto wa England,
Luke Shaw amekamilisha usajili katika klabu ya Manchester United kwa dau
la paundi milioni 31.5 na kusaini mkataba wa miaka minne kukipiga Old
Trafford.
Nyota huyo kinda amefuzu vipimo
vya afya leo katika uwanja wa mazoezi wa Carrington na imetaarifiwa kuwa
atakuwa chaguo la kwanza la kocha Louis van Gaal katika nafasi ya
kushoto.
Inafahamika kuwa kinda huyo
atahakikishiwa nafasi ya kuanza, huku beki mkongwe mwenye miaka 33,
Mfaransa, Patrice Evra ambaye atabakia kwa mwaka mmoja akipunguziwa
majukumu.

Comments
Post a Comment