MTEMVU: WAPINZANI HATA WAKIUNGANA VIPI CCM ITAWABWAGA, ASHANGAA KUAMBIWA ANA MASLAHI BINAFSI KUWATETEA MAMALISHE
Mbunge
wa Temeke, Abbas Mtemvu akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya
Wazazi ya CCM, wilaya ya Temeke, leo katika ukumbi wa Manispaa ya wilaya
hiyo jijini Dar es Salaam.
Mbunge
wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, akimkabidhi hati
ya pongezi , Zaitun Lukinga, ya kuwa kiongozi wa Jumuia ya Wazazi awamu
zaidi ya moja katika nafasi ya Katibu wa Jumuia ya wazazi Kata ya
Kurasini, wakati wa mkutano huo leo
NA BASHIR NKOROMO, TEMEKE
MBUNGE wa Temeke Abbas Mtemvu amewananga wapinzani akisema hata wakisimamisha mgombea mmoja mmoja, katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, CCM itawabwaga.
MBUNGE wa Temeke Abbas Mtemvu amewananga wapinzani akisema hata wakisimamisha mgombea mmoja mmoja, katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, CCM itawabwaga.
Amesema, uhakika huo anao na hata
wapinzani wenyewe wanajua hilo, kwa kuwa hawaizidi CCM kwa weledi wa
kisiasa, kwa akili wala wingi wa wanachama.
Mtemvu amsema hayo wakati
akifungua kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Temeke,
kilichofanyika leo, Juni 27, 2014, kwenye Ukumbi wa Manispaa ya wilaya
hiyo, mjini Dar es Salaam.
“Wapinzani baada ya kuona kuwa
hawatuwezi kwa kila chama kivyake, sasa mnaona wanavyotapatapa, mara eti
huo Ukawa walioanzisha wanataka pia kuutumia kwenye chaguzi, kuweka
mgombea mmoja mmoja kwa wote, mimi bado naamini hata wafanyeje CCM
itawabwaga tu”, alisema Mtemvu.
Mtemvu alisema, pale ambapo
wapinzani wamekuwa wakipenya na kunyakuwa ubunge au udiwani ni pale
ambapo CCM wenyewe wanakuwa wamejichanganya.
“Ikifika acheni mambo ya kuanza
mizozano ya ndani kwa ndani kutokana na makundi ambayo husababishwa na
baadhi ya wagombea au wanachama wanaowataka wagombea kwa lazima,
tukiachana na hili nawahawakikhieni wapinzani hawapati hata kiti kimoja
cha cha mtaa”, alisema Mtemvu.
Mtemvu aliwataka wana-CCM pia
kuachana na mambo ya kushughulika tu na wanaotaka nafasi ambao wana
fedha, akisema, kufanya hivyo kunasababisha baadhi kuwa wagombea
kutokana na uwezo wa fedha tu na siyo wa uongozi.
Aliwataka mtu anapowajia kwa fedha
kuzipokea na kuzila, lakini wakati waanapofikia maamuzi muhimu kwenye
uchaguzi wahakikishe wanachagua yule wanayemfahamu kwa thati kwamba anao
uwezo wa uongozi.
Alisema, wapo baadhi ya wanachama
wa CCM wanao uwezo wa kuongoza lakini hawana fedha, hivyo watu wa aina
hiyo wasitoswe kwa sababu ya ufukara wao.
Mtemvu alisema kiongozi mwenye
uwezo ni yule anayekubalika na watu, saa zote yupo na watu na anajali
maslahi ya wanyonge siyo wale anaowajua kuwa ni wake tu.
“Mfano ni kama hivi tunavyofanya
sasa wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam. Kila mara tunapigania wanyonge,
juzi nimepambana kuwatetea mamalishe wasifukuzwe hovyo, japo baadhi ya
watu tena waliopewa malmaka na Rais waknibeza eti nina maslahi binafsi,
khaa, yaani mimi niwe na maslahi na mamalishe huu kama siyo uzushi ni
nini?” alisema Mtevu.
Comments
Post a Comment