Kocha Mkuu mpya wa Yanga SC
Marcio Maximo (kushoto) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya
klabu ya Yanga, kulia ni msaidizi wake Leonado Neiva
Kocha mbrazil Marcio Maximo leo
amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuwatumikia Mabingwa mara
24 wa Ligi Kuu ya Vodacom timu ya Young Africans pamoja na msaidizi
wake Leonadro Neiva ambao wamesema wamekuja kuisaidia Yanga iweze
kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali.
Akiongea na waandishi wa habari
makao makuu ya klabu ya Yanga, Maximo amesema anajiskia furaha sana
kurudi kufanya kazi Tanzania, kwani watu wake ni wakarimu, wapenda mpira
hivyo anaona kama yupo nyumbani japo awamu hii ni kwa majukumu ya ngazi
ya klabu tofauti na awali alipokua ngazi ya Taifa
Comments
Post a Comment