MSIMU uliopita wa ligi kuu soka
Tanzania bara, Juma Mwambusi wa Mbeya City fc alichaguliwa kuwa kocha
bora wa msimu baada ya kuiongoza klabu hiyo mpya kushika nafasi ya tatu
katika msimamo.
Mbeya City fc walizisumbua klabu
kubwa za Simba na Yanga, hata mabingwa Azam fc. Walimaliza nafasi ya
tatu mbele ya mnyama Simba kwa kujikusanyia pointi 49 kibindoni.
Walishinda mechi 13, wakatoka sare
mechi 10 na kufungwa mechi 3. Walikula kipigo cha kwanza cha bao 1-0
kutoka kwa Yanga ndani ya uwanja wa Taifa. Wakalala 2-0 dhidi ya Wagosi
wa Kaya, Coastal Union, Mkwakwani Tanga. Na mechi ya tatu kufungwa ni
ile ya 2-1 dhidi ya Azam fc.
Mechi hii ilipigwa uwanja wa Sokoine na kimsingi ndio iliamua ubingwa kutua mikononi mwa wana Lambalamba.
Kocha
wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi (katikati) akizungumza na wachezaji
wake Hassan Mwasapili (kushoto) na Peter Richard (kulia).
Mwambusi ni kocha maarufu nchini,
kila timu anayoifundisha inapata mafanikio. Kumbuka alipokuwa na
wajelajela Tanzania Prisons hali ilikuwaje.
Msimu uliopita, Mwambusi alikuja
na kikosi chenye wachezaji wapya kabisa katika michuano ya ligi.
Walikuwa vijana wadogo wasio na uzoefu, lakini aliwaamini kwasababu
alitoka nao ligi daraja la kwanza ambapo alipanda kucheza ligi kuu bila
kufungwa mchezo wowote.
Comments
Post a Comment