Umoja wa Mataifa umeelezea ghadhabu kutokana
na Fatwa iliyotolewa na Kundi la wapiganaji wa
Kiislamu wa ISIS ya kuwataka wanawake wote
waliozidi umri wa miaka 11 kukeketwa.
Afisa wa shirika la umoja wa mataifa nchini
Iraq ,Jacqueline Badcock ameonya kuwa agizo hilo
la kidini ama Fatwa itawaathiri zaidi ya wanawake
milioni nne kati ya umri wa miaka 11-46.
Kundi hilo la wapiganaji wa Kiislamu ndilo
linaongoza mashambulizi katika maeneo ya
Kaskazini mwa Iraq na wao ndio wanaotawala mji
wa Mosul.
Kundi hilo linalosheheni wapiganaji wa dhehebu la
Sunni ndilo linaloendeleza wimbi la mashambulizi
katika taifa hilo linalotishia kusambaratika katika ya
maeneo yanayotawaliwa na madhehebu.
Ukeketaji sio kawaida nchini Iraq.
Mapema juma hili, Isisi iliwalazimisha Wakriso
katika mji wa Mosul kuondoka na kuandika herufi N
kwenye nyumba zao, hatua ambayo imetambuliwa
kama kutaifisha mali za Wakristo katika eneo hilo.
Kulingana na amri hiyo mpya iliyotolewa chini ya
Sharia, , wanawake wote kati ya umri wa miaka 11
na 46 wanapaswa kukeketwa.
ISIS yaagiza wanawake wote kuanzia umri wa
miaka 11-46 kukeketwa.
Bi Badcock alisema kuwa utamaduni huo ni jambo
geni sana nchini Iraq na ni swala linalopaswa
kujadiliwa.
Alisema hayo alipokuwa akiwahutubia waandishi wa
habari kupitia simu ya video katika mji mkuu wa
Mkoa wa Kurdi wa Ibril.
Zoezi hilo la kuwapasha tohara wanawake
limeenea sana katika mataifa mengi ya Afrika
mashariki ya kati na jamii kadhaa barani Asia.
Baraza la Umoja wa mataifa lilipitisha mswada
mnamo mwaka wa 2012 ya kuharamisha tamaduni
hiyo ya upashwaji tohara kwa wanawake.
Isis ilitwaa mji wa Mosul mnamo mwezi wa Juni
miongoni mwa miji mingine midogo midogo
kuelekea mji mkuu wa Baghdad.
Comments
Post a Comment