Mkuu wa manjago alikwenda acha gari lake
lioshwe sehemu fulani. Aliporudi akagundua haioni
laptop yake. Akawapigia askari wake wakaja
wakawakusanya waosha magari wote pale jirani
na kuondoka nao. Kesho yake asubuhi mkuu
akapigiwa simu na Mchepuko wake kumkumbusha
kuwa toka jana yake alikuwa kaacha laptop. Mkuu
ndio akakumbuka kosa lake akawapigia askari
wake na kuwaambia wawaachie wale waosha
magari. Askari wakamjibu, 'Mkuu mbona
umechelewa? Wote tumeshawapeleka
mahakaman maana baada ya kuwahoji usiku
kucha wamekubali kuwa waliiba hiyo laptop na
wameshaiuza kwa mfanya biashara wa Kizambia.
Comments
Post a Comment