Chama cha Madaktari nchini Tanzania kimelaani
kitendo cha kutupwa kwa viungo vya binadamu nje
ya jiji la Dar es Salaam kinyume cha sheria.
Rais wa chama hicho, Dk. Primus Saidia ametaka
hatua madhubuti zichukuliwe dhidi ya wahusika
ikiwemo kupigwa marufuku kwa mtu au taasisi
iliyohusika kuendesha shughuli zozote za utafiti
kwa kutumia viungo vya binadamu.
Dk Primus ameweka bayana kwamba, licha ya fani
hiyo ya udaktari kuruhusiwa kutumia viungo vya
binadamu katika shughuli mbali mbali za utafiti kwa
mujibu wa sheria za kitaifa na kimataifa lakini
ameelezea kwamba kitendo hicho kimekiuka haki
za binadamu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za
Chama hicho cha madaktari hapa jijini Dar es
Salaam, kiongozi huyo ametaka hatua madhubuti
zikuchuliwe dhidi ya wahusika ikiwemo kufungiwa.
Sakata la kutupwa kwa viungo hivyo kinyume cha
sheria katika mji wa Mbweni nje ya jiji la Dar es
Salaam siku mbili zilizopita, lilizua taharuki
miongoni mwa watu wa kada mbalimbali.
Tayari watu wanane kutoka Chuo cha udaktari cha
IMTU kilichopo hapa jijini Dar es Salaam
wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusishwa
kwa kutupwa kwa viungo hivyo ambavyo viliwekwa
katika mifuko ya plastiki ipatayo 85.
Comments
Post a Comment