Kocha mkuu wa Simba sc, Mcroatia, Zdravko Logarusic (wa kwanza kushoto)
HAKUNA uchawi katika soka!. Kabumbu ni mipango na kupita njia sahihi ili kufikia kiwango cha juu.
Tanzania ni miongoni mwa nchi `tia
maji tia maji` kwenye mipango ya soka. Viongozi na mashabiki wanataka
kupita njia ya mkato `short cut` ili kupata mafanikio.
Moja ya kosa kubwa wafanyalo watu
wengi ni kulifananisha soka letu na mataifa yaliyoendelea (barani Ulaya
na Amerika). Utasikia mbona hata Chelsea, Man United, Barcelona
wanafukuza makocha?, wanaacha wachezaji?.
Kumbe klabu hizi zina mipango na
zimekamatwa na wafanyabiashara ambao wamewekeza pesa zao. Hakuna mfanya
biashara atayevulimilia hasara. Mtu anainunua klabu kwa mabilioni ya
fedha, mfano Roman Abramovich wa Chelsea. Hawezi kuona kocha anavurunda
na kumuacha, lazima achukue hatua kwasababu anataka faida.
Pia
klabu za Ulaya, mara nyingi kazi ya kocha ni kutengeneza timu
kiuchezaji, (ufundi na mbinu za mpira). kwa asilimia kubwa, wachezaji
wanaowakuta wanakuwa tayari wameandaliwa vizuri au ananunua wachezaji
waliopikwa tayari. Kwa maana ya kwamba, wana misingi ya mpira, kazi
yake inabaki kuunganisha timu kwa kutumia wachezaji walio tayari kufanya
kazi.
Kama kazi yako ni kuufundisha
mpira na kuunganisha wachezaji katika falsafa yako, yaani wachezaji wote
ni wazuri, inashindikanaje kufukuzwa unaposhindwa kuwapa mbinu sahihi
za mpira?. Ndio maana makocha wengi Ulaya wanawajibishwa kwa kushindwa
kuipa mbinu za uhakika timu yake
Comments
Post a Comment