Skip to main content

Tahadhari Kuhusu Kuingilia Au Kufuatilia Mawasiliano Ya Watu


TAARIFA KWA UMMA
TAHADHARI KUHUSU KUINGILIA AU KUFUATILIA MAWASILIANO YA WATU
***
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa Programu (Application) ya simu ikijulikana kama SOFTBOX TANZANIA iliyosemekana iko kwenye Google PLAYSTORE.

Ilidaiwa kuwa program (Application) hiyo ya SOFTBOX TANZANIA ilikuwa na uwezo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi.

Kwa yeyote aliyekuwa na nia hiyo ya kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu mwingine alihitajika kulipia fedha kiasi cha Tshs 35,000/= kupitia mitandao ya simu ili kupata namba ya siri kwa ajili ya kuwezesha nia hiyo.

Mamlaka ya Mawasiliano imefanya uchunguzi kubaini kuwepo kwa programu hiyo na ukweli kuhusu uwezo wake wa kufanya kilichodaiwa, ikiwa ni pamoja na kuangalia madhara ya program hiyo na sheria inasema nini kuhusu suala hili.
 
Baada ya kufanya uchunguzi wa kina, Mamlaka ya Mawasiliano ilibaini na imejiridhisha kuwa program (Application) hiyo haina uwezo huo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi kama ilivyodaiwa.

Aidha Mamlaka imebaini kuwa watengenezaji (Developers) wa programu hiyo walikuwa na nia ya kutapeli na kujipatia fedha hiyo kiasi cha Tshs 35,000/= kwa njia ya udanganyifu wakitumia kivutio cha kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu za watu binafsi.

Programu (Application) nyingine ya aina hiyo iliibuka tena ikiitwa SIMNET Tanzania ikiwa na maelezo kama ya awali.

Wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania pamoja na Jeshi la Polisi wakiendelea na uchunguzi zaidi, tunapenda kuuarifu umma wa Watanzania kuepuka kufanya mambo yafuatayo:

1. Kuvutiwa na matendo yaliyo kinyume na sheria na maadili ya matumizi mazuri ya mawasiliano kama hili la kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi. 
 
Kitendo hiki ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 6 na 10 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 na kifungu cha 123 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya Mwaka 2010. 
 
Sheria katika vifungu hivyo inakataza mtu yeyote kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine. Adhabu kali ya makosa haya ni faini isiyopungua shilingi milioni tano au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.

2. Mamlaka inawatahadharisha watumiaji wa huduma za mawasiliano kutokuwa wepesi na kudanganyika kufanya malipo yoyote kwa njia ya mitandao kwa huduma wasiyokuwa na uhakika nayo au bila kujiridhisha na uwepo wa huduma hiyo.
 
 Ni vizuri kutoa taarifa kwa mtoa huduma wako au kuwasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano kupitia barua pepe malalamiko@tcra.go.tz au kupiga simu namba 0784558270/1.
 
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
04/12/2015.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...