Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (UDSM) Bashiru Ally |
Tanzania ipo kwenye kipindi cha mpito: kijamii, kiuchumi na kisiasa. Kila mwenye uwezo wa kutafakari, ana cha kusema kuhusu mustakabali wa taifa hili.
Watu wengi, kupitia njia mbalimbali za mawasiliano, wanatoa tafakuri zao kuhusu suala hilo. Mmoja wa watu hao ni Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa katika Chuo kikuu cha Dar es salaam, Bashiru Ally ambaye anasema, “Ninapotazama Tanzania ijayo, ninaona giza totoro.
Tofauti na watu wengi, hataki kuzungumzia kasoro zinazojitokeza katika mchakato wa kuunda Katiba mpya, akisema kinachotokea ni matunda ya mbegu zilizopandwa.
Akifafanua kauli hiyo, anasema; “Tanzania haikuwahi kuandika Katiba kwa kushirikisha wananchi kwa njia ya moja kwa moja. Kazi hii haiwezi kutekelezwa kwa mara ya kwanza, ndani ya miaka miwili mpaka mitatu na endapo hilo litatokea, yatakuwa maajabu ya dunia.”
Mtaalamu huyo wa masuala ya siasa nchini anasema, taifa limegawanyika kisiasana kimatabaka. Wanaofaulu ni wachache ikilinganishwa na wanaoshindwa katika mitihani shuleni, hakuna anayejali wanakoishia.
Kadhalika hali ya kiuchumi imewagawa wanajamii katika matabaka. “H ishara nzuri kwa taifa linalosifika kuwa na utengamavu wa miaka mingi; inahitaji umakini, hekima na busara za kiwango cha juu kukabiliana nayo,” anaeleza Ally.
Anaendelea kueleza kuwa “vuguvugu la mambo yote hayo likichanganywa na mchakato unaoendelea nchini, unaoelezwa kuwa na lengo la kuunda Katiba mpya, inayotarajiwa kuongoza taifa kwa miaka kati ya 50 na 100 ijayo, wakati hali halisi inayoonekana ni uundwaji wa Katiba kwa ajili ya kulinda maslahi ya kundi fulani katika jamii, ni dhahiri kuwa nchi inaweza kukabiliwa na magumu mbeleni.”
“Ukweli vyama vya siasa vinaburuza kila mtu, ili mradi ifikapo Aprili, 2014 Katiba wanayoitaka ipatikane, wakipuuza hali halisi kuwa Katiba inayohitajika ni yenye maslahi kwa Watanzania wote, wa kizazi kilichopo na kijacho,”
Ally anasema kila kitu katika mchakato wa Katiba mpya kinafanyika kwa haraka ya ajabu. “Hata sheria inayosimamia mchakato mzima wa uundwaji Katiba hiyo, imetungwa kwa haraka kama ilivyotungwa Sheria ya Kuzuia Ugaidi au ile ya Kubinafsisha Benki ya Biashara ya Taifa,(NBC).
Ally anabainisha kuwa kilichofanywa na vyama vya siasa ni kukurupukia hoja ya Kuunda Katiba mpya, huku vikizingatia zaidi maslahi yake na kuweka kando hali halisi; ndiyo maana vimekuwa vikivalia njuga kila hatua ya mchakato huo, vikilenga kuhodhi haki za wengine.
“Matokeo ya vitendo hivyo yanaelezwa na mhadhiri huyo kuwa ni taifa kupata Katiba itakayotokana na wenye nguvu; ambao anasema kuwa bila shaka ni Chama cha siasa kilicho madarakani, (CCM),” anasema.
Nini kifanyike?
Ally anataja njia pekee iliyobaki, anayoamini kuwa italeta mabadiliko yatakayolinusuru taifa dhidi ya machafuko kwamba ni walioshika mpini, kuweka mbele msalahi ya taifa.ii siyo
Ally anataja njia pekee iliyobaki, anayoamini kuwa italeta mabadiliko yatakayolinusuru taifa dhidi ya machafuko kwamba ni walioshika mpini, kuweka mbele msalahi ya taifa.ii siyo
Comments
Post a Comment