Katika hotuba hiyo iliyohaririwa, Profesa Kahigi alisema baadhi ya maofisa wa idara hiyo wamekuwa wakitajwa kwenye vyombo vya habari kuhusika na uhalifu huo, lakini Serikali imekaa kimya.
Wasema inajihusisha kwenye vitendo vya utekaji na utesaji watu wanaoikosoa Serikali
Kambi Upinzani Bungeni imeitaka Serikali kuwachukulia hatua maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa – Ikulu ambao wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu vya utekaji na utesaji kwa watu wanaoonekana kuikosoa Serikali.
Madai hayo yalitolewa bungeni juzi na msemaji wa kambi hiyo, kuhusu Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Profesa Kulikoyela Kahigi, katika hotuba ambayo awali ilizua mvutano wa mambo gani yasomwe na yapi yabaki.
Ilibidi hotuba hiyo iahirishwe kwa muda, hadi kamati ya kanuni ikutane na kutoa uamuzi kwamba baadhi ya mambo yanayotaja majina ya watumishi wa usalama wa taifa na mengine yaliyoko mahakamani yaondolewe.
Katika hotuba hiyo iliyohaririwa, Profesa Kahigi alisema baadhi ya maofisa wa idara hiyo wamekuwa wakitajwa kwenye vyombo vya habari kuhusika na uhalifu huo, lakini Serikali imekaa kimya.
Alisema iwapo watuhumiwa hao wangekamatwa na kuchukuliwa hatua, utekaji na utesaji wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri wa New Habari Ltd. ungeweza kuepukika.
Mbunge huyo alisema mazingira ya kuteswa kwa Kibanda ya kung’olewa kucha, meno na kutobolewa jicho yanafanana na yale yaliyohusishwa na usalama wa taifa.
Mbunge huyo alisema mazingira ya kuteswa kwa Kibanda ya kung’olewa kucha, meno na kutobolewa jicho yanafanana na yale yaliyohusishwa na usalama wa taifa.
Mbunge huyo alinukuu Sheria ya Ujasusi na Usalama ya Tanzania (Tanzania Intelligence and Security Services Act) ya 1996, sehemu inayozuia idara hiyo kufanya upelelezi wa ufuatiliaji - “ushushushu” kwa watu wanaoipinga Serikali kwa misingi ya kisheria na kikatiba.
Sehemu hiyo Ibara ya 5(2), kipengele ‘a’ na ‘b’ ambayo Profesa Kahigi alisema imekuwa inavunjwa na Idara hiyo, inasema, “Haitakuwa kazi ya Idara kutekeleza hatua za usalama au kufanya upelelezi wa ufuatiliaji wa mtu yeyote au kundi lolote la watu kwa sababu tu ya kuhusika na kupinga jambo halali kuhusiana na jambo lolote la kikatiba, sheria au Serikali ya Tanzania”.
Hata hivyo Serikali imekanusha.
Comments
Post a Comment