Jumapili, 5 Julai 2015
- Maono ni taarifa inayokuja kwa mtu katika hali ya ukamilifu.
- Maono ya wakristo waamini walio wengi yamezama yaani yamepoteza mwelekeo, kwa sababu wakristo sana sana jamii ya waaminio hawaweki bidii ya kuishi maisha ya ukweli.
- kila mwanadamu mwenye mwili Mungu amempa kipawa yaani karama, katika hili kinacho leta shida ni wakristo kutokuweka bidii ya kuchochea karama zao, mara nyingi jambo hili husababisha kina cha maarifa ya rohoni kujifunga na hapo huwa ndio mwanzo wa Maono ya mkristo kuzimika.
- ( Kinacho linda Maono ya mkristo ni bidii aliyonayo katika kujifunza Neno la Mungu )
- Mkristo anaye mcha Mungu katika hali ya maono mara nyingi safari yake huwa salama kwa sababu maono ni mwongozo sahihi katika maisha ya mtu anaye mwamini Mungu.
- ( Kanisa linahitaji maono ili Liwe salama )
- Ili niweze kuyafikia maono yangu inatakiwa nipingane na mambo yafuatayo katika maisha yangu:-
i).Nisiruhusu moyo Wangu kubeba hila
Ii).Wivu
iii).Chuki
iv).Tamaa ya mwili
v).Tamaa ya mali
- Haya mambo 5 ndiyo yanayo gharimu kwa sehemu kubwa kudidimiza maono ya wakristo walio wengi.
- Waefeso 4: 17- 32
- (Moyo wa mkristo ukifa ganzi, hapo ndipo anguko la mkristo linapoanzia,na ganzi katika moyo wa mkristo Huja katika mazingira haya,huja katika mazingira ya roho ya kiburi)
- Roho ya kiburi ikisha uvalisha moyo wa mwamini ganzi mwamini huyo atakumbwa na mambo yafuatayo :-
1.Hawezi kukubali ushauri wa mtu yeyote, maana yake kila kitu anajua.
2.Hata angeshirikishwa zuri namna gani kwake halina maana, hapo ndipo (hila) ilipo.
- Kanuni ya Mungu jinsi ilivyo huvitumia vitu vilivyo dharaulika kuonya ndio maana wazimu wa balaamu ulitulizwa kwa kinywa cha punda.
- ( Maono ya mkristo yanalindwa na hekima itokayo ndani ya Neno la Mungu )
- Maono ndio njia sahihi ya kuliongoza kanisa katika ukweli, ndio maana shetani hupambana sana na makanisa yenye maono ili ayabomoe.
- Inatakiwa niyalinde maono niliyo nayo kwa gharama yoyote kwa sababu kama nikizembea maono niliyo nayo yakazimwa huwa hayajirejei tena.
- Suala la kuokoa maono yangu ni jukumu langu mimi binafsi kwa sababu mimi ndiye ninaye tambua uthamani wa maono niliyo nayo.
- Ili niweze kuyatunza maono niliyo nayo inatakiwa nidumu katika sheria ya Bwana, jambo hili hata Mithali imelisema. Mithali 3:1-2
MAMBO YA KUFANYA ILI NIDUMU KATIKA MAONO
-Jambo la kwanza litakalo nisaidia mimi kama mwamini ili niweze kuyalinda maono yangu ni kuruhusu moyo wangu kukubaliana kuendana na maisha yaliyo andikwa ndani ya Biblia.
Comments
Post a Comment