Yaani ndio nimetokea hapo kwake kwani ni ajabu kabisa.Alikuwa na girl friend wake kwenye gari kufika eneo la Mount Meru akagonga Hiace kwa nyuma gari ikabonyea lakini yeye na mpenziwe wakatoka wazima bint anadai baada ya dakika km 2 akahisi kizunguzungu akaanguka chini kuja kushtuka anaona watu wengi na kijana naye kutoka hapo akatimka mpaka karibu na nyumbani kwake ndio kujipiga risasi na kufa.Sasa bint anaulizwa mlikuwa na ugomvi anasema wala yeye mwenyewe anashangaa kilichomkuta keshatoka mzima kwenye ajali kukimbia na kwenda kujiua.Ni kijana wa 86 yaani mdogo kabisa na ndio pesa imekubali na baba yake ni mgonjwa yuko hoi muda huo yenyewe alikuwa amepigiwa cmu na dada zake aende kumuogesha maana ni mtt pekee wa kiume na ndio alikuwa anaenda sasa hawajui ni kitu gani kilimkumba kuamua kujiua
Kz Baba Precious Acasolid
tunazidi kupamabana kupata taarifa zaidi endelea kutufuatilia...............Mfanyabiashara wa madini, Richard Lucas (29) anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi kichwani baada ya kusababisha ajali mbili tofauti.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema alijipiga risasi juzi saa 12:45 jioni nyumbani kwake eneo la Kimandolu. Alitumia bastola aina ya Luger yenye namba B136986. Alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa Lucas alitokea Tengeru akiwa na gari aina ya Toyota Rav 4 yenye namba za usajili T 494 CKY alikokuwa amemfuata rafiki yake aliyekuwa amepata ajali ya kugongwa na gari.
Alipofika eneo la Sekei Darajani, alimgonga mwendesha pikipiki na kuendelea na safari. Mbele kidogo, kwa mujibu wa polisi, aligonga daladala lenye namba za usajili T 636 CUR aina ya Nissan iliyokuwa inachukua abiria.
Baada ya hapo gari ya Lucas ilipinduka na waliokolewa kwa kupitia dirishani na wananchi.
Inadaiwa alitoka eneo la tukio kwa pikipiki ya kukodi kwenda nyumbani kwao Kimandolu huku akimwacha Vick Mchuma kwenye eneo la tukio.
Alisema baada ya muda, Mchuma ambaye waliongozana naye kwenda kumsaidia rafiki yao aliyepata ajali Tengeru, alipata taarifa kuwa Lucas amejipiga risasi na mwili upo Hospitali ya Mount Meru. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo
Comments
Post a Comment