Stori: Na Francis Godwin, Iringa
KUFUATIA kifo cha Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Dk. Wiliam Mgimwa aliyefariki katika Hospitali ya Kloof Med- Clinic, Pretoria, Afrika Kusini wiki iliyopita na anayetarajia kuzikwa leo Kalenga, jimbo zima limezizima kwa simanzi.
KUFUATIA kifo cha Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Dk. Wiliam Mgimwa aliyefariki katika Hospitali ya Kloof Med- Clinic, Pretoria, Afrika Kusini wiki iliyopita na anayetarajia kuzikwa leo Kalenga, jimbo zima limezizima kwa simanzi.
Wananchi wa jimbo hilo wameingiwa na simanzi kwa kuwa enzi za uhai wake marehemu alikuwa karibu sana na wapiga kura wake na hata maisha yake aliyokuwa akiishi ni tofauti na baadhi ya viongozi ambao wanalalamikiwa kwa kuwatelekeza wananchi wao baada ya kupanda vyeo.
“Natambua ni mapenzi ya Mungu ila kweli tulimpenda sana mbunge wetu alikuwa ni mtu wa kujishusha, asiyependa kujilimbikizia mali zaidi ya kuwatumikia wananchi ....kweli kifo chake ni pigo kubwa,” alisema mmoja wa wapiga kura wake aliyejitambulisha kwa jina la Dismas Mbwela.
Gazeti hili lilifika nyumbani kwa marehemu eneo la Magunga Jimboni Kalenga ambapo liliiona nyumba yake ambayo ni ya kawaida ukilinganisha na nyumba za wananchi wa kawaida na ni vigumu kuamini kama hapa ndipo nyumbani kwa waziri wa fedha, hali inayoonesha kuwa alikuwa mwadilifu kama hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere ambaye alikuwa akiwajali wananchi.
Katika kijiji hicho, hali ya huzuni imetanda na maandalizi ya mazishi ikiwa ni pamoja na sehemu atakapopumzishwa imeshaandaliwa. Mwenyekiti wa mazishi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christina Ishengoma na kamati yake wamekuwa kijijini hapo kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
Comments
Post a Comment