Kama uliwahi kuweka vocha kwenye simu yako alafu ukakuta ile hela uliyoweka haipo na wala hujaitumia, hii ishu imewagusa Wabunge… Alianza Mbunge kwa kuuliza swali kwamba nini kinafanyika kuzuia wizi wa aina hiyo.
“Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba wanapoteza pesa kujiunga na vifurushi ama wanaponunua vocha… Serikali itachukua hatua gani kudhibiti Makampuni ya simu ambayo yanafanya wizi kwa wananchi” >>> Mbunge Murtaza Mangungu.
“Kumekuwa na udhaifu mkubwa kwa upande wa TCRA kwenye kufuatilia malalamiko ya watu pale ambapo wanadhurumiwa, watu wanatoa malalamiko kwa Makampuni ya simu lakini hakuna hatua zinazochukuliwa” >> January Makamba.
“Serikali imetoa onyo kwa TCRA kwamba tunataka hatua zianze kuchukuliwa na namna mpya ikiwemo kuhakikisha kwamba kuna kituo ambacho kipo saa zote kwa ajili ya kupokea simu na malalamiko ya watu na ni rahisi kituo hicho kufikika na watu wanahakikishiwa majibu, malalamiko yasiposhughulikiwa ndani ya saa 48 hatua za Kisheria zinachukuliwa kwa makampuni ya simu” >>> Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Comments
Post a Comment