Baada ya kuripotiwa ugonjwa wa Kipindupindu kutokea katika maeneo mbalimbali kanda ya Ziwa headlines zimerudi tena.
Uchunguzi uliofanywa na Maabara ya chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA umethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya nguruwe katika Wilaya ya Nyamagana, Mwanza.
Katika taarifa iliyotolewa na Katibu tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mwanza, Yohana Sagenge amethibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo ambao unasababishwa na Virusu aina ya African Swine fever Virus ambapo madhara yake ni makubwa na husababisha kifo kwa 100%. kwa wanyama hao.
Taarifa hiyo ilisomeka hivi
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAAOFISI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA
TAARIFA KWA UMMA. YAH: MLIPUKO WA UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE
Kumetokea mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Nguruwe (African Swine Fever) Wilaya yaNyamagana, Kata za Mabatini, Mirongo kishiri na Buhongwa na Igoma. Mlipuko huuumedhibitishwa kwa uchunguzi uliofanyawa na Maabara ya Chuo kikuu cha Kilimo chaSokoine (SUA)Ugonjwa wa Homa ya Nguruwe unasababishwa na Virusi (African Swine fever virus).Madhara yake ni makubwa kwa wafugaji na kiuchumi kwani husababisha vifo asilimia100 (100%) kwa Nguruwe wote walioambukizwa.Ugonjwa wa Homa ya Nguruwe
hauna chanjo wala tiba na hauambukiziBinadamu.
Njia pekee ya kudhibiti ugonjwa huu ni kuzuia kueneoa kwa maambuzitoka eneo lenye maambukizi kwenda eneo lisiloambukizwa.
HATUA ZA TAHADHARI KUZUIA KUENEA KWA UGONJWA WA HOMA YANGURUWE
Wafugaji waepuke kununua Nguruwe kutoka kwenyeMaeneo/Mashamba yenye ugonjwa
Nguruwe wafugwe kwenye Mabanda imara na waepukekutembea ovyo
Nguruwe wasilishwe mizoga au masalio ya chakula kutokavyanzo visivyojulikana
|
Comments
Post a Comment