Skip to main content

Ajira za makatibu wakuu ziko salama- Ikulu


Uamuzi wa Rais John Magufuli kuunganisha wizara kutoka 30 hadi kuwa 18 na idadi ndogo ya mawaziri, hautasababisha kupunguzwa kwa watumishi, hasa makatibu wakuu, Ikulu imeeleza.

Juzi, Rais Magufuli alitangaza kuunganisha wizara na kuunda Baraza la Mawaziri lenye wizara 18 kutoka 30 za Serikali ya Awamu ya Nne, uamuzi ambao umeibua hofu kwa baadhi ya watumishi kuwa panga hilo linaweza kuwakumba makatibu wa wizara zilizopunguzwa.

Jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alieleza kuwa Serikali itafanya mgawanyo mpya wa majukumu kwa watumishi wote na suala la kuwapunguza kazi halifikiriwi kwa sasa.

Balozi Sefue alisema fedha zilizotengwa kwenye bajeti ya mwaka 2015/16, zitapelekwa kwenye kila wizara husika, hata kama itakuwa imeungwanishwa na nyingine na kuunda wizara moja.

Katika mabadiliko na uundaji wa baraza hilo, Dk Magufuli ameunganisha baadhi ya wizara, huku akizihamisha baadhi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na kuzipeleka Ofisi ya Rais na nyingine kuziondoa kwenye kujitegemea na kuziingiza Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kwa hatua hiyo, watumishi wa wizara kati ya mbili hadi tatu watajikuta wakiwa katika wizara moja pamoja na waliokuwa makatibu wakuu wa wizara hizo, jambo litakaloongeza idadi ya watumishi na baadhi yao huenda wakajikuta wakifanya kazi zinazofanana au kukosa kitu cha kufanya.

“Baada ya baraza kuundwa lazima kutakuwa na realignment ya watumishi (kuunganisha upya shughuli zinazoshabihiana). Kuna mambo mengi, hata ofisi inabidi tuzipange upya. Hiyo ipo wazi kwa watumishi, sidhani kama kuna ulazima wa kupunguza idadi yao zaidi ya kuwapangia majukumu mengine,” alisema Sefue.

Alisema mtumishi wa umma hajaumbwa kuwa mtumishi wa wizara moja tu maisha yake yote.

“Kwa hiyo, tutatazama kama wanaweza kuwa redeployed (kupangwa upya) vipi. Wale ambao hawatahitajika kwa ukubwa wa baraza la mawaziri lililopo, tutaona wanaweza kutumika vizuri zaidi sehemu gani,” alisema.

Alipoulizwa kama kuna utaratibu wowote wa kupunguza wafanyakazi alisema: “Hatupunguzi, labda tuone mtu hahitajiki kabisa. Lakini, kwa wakati huu hatuna msingi wa kusema kuna watu hatutawahitaji. Baada ya mawaziri kuapishwa na kuanza kazi tutaanza suala hili.”

Kuhusu makatibu wakuu wa wizara ambazo zimeunganishwa na kuwa wizara moja, Balozi Sefue alisema: “Nao ni hivyo hivyo. Bado kuna mambo mengi ambayo wanaweza kupewa na wakafanya vizuri tu, wakati wa uamuzi huo bado haujafika ila kwa sasa hatufikirii kuwapunguza.”

Kuhusu mpangilio wa majukumu yao, Balozi Sefue alisema: “Ngoja uundwaji wa baraza ukamilike tuone wapi watahitajika na hao ambao watabaki tuwafanye nini. Uamuzi huo utafanyika baadaye.”

Akizungumzia mgawanyo wa fedha za bajeti za wizara ambazo kwa sasa zimeunganishwa na kuwa wizara moja, katibu huyo mkuu kiongozi alisema bajeti ya Serikali ni kwa vitu maalumu, kwa hiyo kama kulikuwa na bajeti ya Wizara ya Afrika Mashariki ambayo katika bajeti walikuwa na kazi inayohusu eneo hilo, fedha ya bajeti hiyo itakwenda inakohitajika kwa ajili ya kufanya kazi iliyokusudiwa licha ya wizara hiyo kuunganishwa.

“Yaani, fedha hiyo itakwenda katika wizara mpya (iliyounganishwa na nyingine), bajeti nayo itakwenda huko sanjari na wafanyakazi ambao nao watakuwa katika wizara hiyo hiyo. Kwa maana hiyo, bajeti hiyo itatumika kama kawaida,” alisema.

Rais Magufuli alisema wakati akitangaza baraza lake la mawaziri kuwa ameamua kuwa na wizara chache ili kuepuka matumizi makubwa ya fedha za Serikali.

Kutokana na uamuzi huo, wizara zilizounganishwa ni ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Utumishi na Utawala Bora, imeunganisha shughuli za Tamisemi zilizokuwa Ofisi ya Waziri Mkuu. Awali, Ofisi ya Rais ilikuwa na waziri watatu; Utawala Bora, Mahusiano na Uratibu na Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Nyingine ni Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambazo zilikuwa mbili tofauti, chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

Katika Ofisi ya Waziri Mkuu, ipo Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu. Awali, Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira ilikuwa inajitegemea, wakati ya walemavu ni mpya.

Mabadiliko hayo yamepunguza idadi ya wizara zilizokuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo ni Sera, Uratibu na Bunge, Uwekezaji na Uwezeshaji na Tamisemi, zikiwa na mawaziri watatu na manaibu wawili.

Nyingine ni Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambazo awali kila moja ilijitegemea.

Wizara ya Fedha sasa imeongezewa Mipango na sasa itaitwa Wizara ya Fedha na Mipango. Pia, Wizara ya Viwanda na Biashara imeongezewa Uwekezaji. Suala la masoko limeondolewa wakati Uwekezaji ilikuwa pamoja na uwezeshaji.

Kutakuwapo pia na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ambayo imeunganisha wizara mbili; Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na ile ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Nyingine ni Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, ambayo imechukua majukumu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na ile ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni matokeo ya kuunganisha Afya na Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
SOURCE:
Mpekuzi blog

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

Tazama picha za utupu ya Mwimbaji wa nyimbo za injili

Hili nalo ni tukio la kushitua baada ya msanii wa nyimbo za injiri kuamua kuanika picha zake za utupu kunako mitandao ya kijamii tukio hili limetokea hivi karibuni Nchini Nigeria Baada ya mwimbaji wa nyimbo za injiri kuweka piha na video kwenye mtandao anajulikana kwa jina la Maheeda  I doubt if this Naija female singer called Maheeda could still be described as a gospel singer giving her acts in recent times, especially in the social media. Her latest show of shame is posting videos of herself in the n*de while taking her bath. Check out more of her craze below: