Skip to main content

Serikali Yaelekeza Uendeshaji wa Sekondari Zake za Bweni


SERIKALI inatarajiwa kutoa utaratibu wa namna wanafunzi wa shule za Serikali za mabweni, watakavyosoma huku ikionya wakuu wa shule watakaodai ada au michango ya aina yoyote, kwamba watachukuliwa hatua ikiwemo kufukuzwa kazi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini amesema hayo jana wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa mwaka wa wadau wa Camfed unaofanyika mjini hapa.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Idara ya Usimamizi wa Elimu, Benard Makali, Sagini alisema kuanzia Januari 2016, elimu nchini katika shule za msingi na sekondari itatolewa bure.

Alisema shule zenye hosteli kisheria, usajili wake ni shule za kutwa na zitapewa utaratibu wake katika uendeshaji na Serikali itakaa na kutoa maelekezo sahihi ili wazazi wasaidie kuchangia chakula.

Amesema Serikali itakaa na kutoa maelekezo sahihi, ili wazazi wasaidie mipango mizuri ya halmashauri. 
 
“Chakula si pesa kama wazazi watakubaliana kuchangia chakula wakati wa mavuno hiyo itakuwa sawa lakini serikali itatoa maelekezo,” alisema.

Alisema kila halmashauri inaweza kuwa na utaratibu wake juu ya suala hilo. Alisema shule hizo wanafunzi wake hawatalipa ada wala michango yoyote lakini wazazi watalazimika kuwanunulia wanafunzi sare, madaftari na usafiri wa kuwapeleka na kuwarudisha nyumbani wakati wa likizo.

Makali alisema awali wanafunzi walikuwa wakilipa ada ya Sh 70,000 kwa mwaka lakini hawatalipa tena ada wala michango yoyote. 
 
“Taratibu zimeshafanywa na shule zitafunguliwa kwa wakati na hakuna mwanafunzi atakayelipa ada au mchango wa aina yoyote” alisema.

Alipohojiwa ni kwa jinsi gani huduma katika shule za bweni zitaboreshwa ikiwemo kuwalipa wapishi na walinzi ambao kwenye maeneo mengi hawajaajiriwa na serikali, Mkurugenzi huyo alisema masuala yote yatatolewa ufafanuzi. 
 
Akizungumzia tatizo la utoro limekuwa likirudisha nyuma maendeleo ya watoto wengi.

“Ukimuuliza Ofisa Wilaya anasema mwamko mdogo wa wazazi, hivi hao wazazi wanaowasingizia siku zote wako nchi nzima?" Alisema. Aliwataka maofisa elimu kufanya kazi zao na si kuwasingizia wazazi.
 
 “Tunapoteza watoto wengi, wanazurura tu sioni kwa nini suala hili linaendelea, mtoto asipoonekana shuleni mwalimu asikae kimya,”alisema.

Alisema sasa watachukua hatua kali kwa walimu atakaozembea suala la utoro kwa wanafunzi. Pia alilipongeza shirika hilo kwa kusomesha watoto wa kike walio katika mazingira magumu na kuwa serikali itaunga mkono juhudi hizo. 
 
Awali, Mkurugenzi wa Camfed Tanzania, Lydia Wilbard alisema watoto 48,373 wameweza kufikiwa na shirika hilo.

Aidha shule 120 zimefikiwa kwa kuboresha mazingira ya shule. Akichangia katika mkutano huo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kilolo iliyopo mkoani Iringa, Seraphina Chodota alisema tafsiri ambayo wananchi wamepata kila kitu kitakuwa gharama ya serikali

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...