Jeneza la mwili wa mtoto ambalo lilikutwa limetelekezwa mbele ya mlango wa mgahawa wa Ester.
---
---
JENEZA lenye mwili wa mtoto mchanga, limezua taharuki kwa wananchi na wakazi wa
Mtaa wa Ihago, Kata ya Mahina, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.
Tukio hilo la kushangaza na la aina yake, lilitokea Agosti
29, mwaka huu, majira ya saa 12:00 asubuhi baada ya kugunduliwa na
mfanyabiashara Ester Musa (28) likiwa limetelekezwa kwenye mlango wa
mgahawa wake.
Jeneza likiwa limefungwa tayari kwa kwenda kuzika mara ya pili.
--
--
Jeneza hilo linaaminika kufukuliwa na watu wasiofahamika kwenye moja ya makaburi eneo la Mahina jijini hapa.
Akizungumza kuhusiana na tukio hilo, Ester anayemiliki na kuendesha mgahawa alisema, alifika katika eneo lake
hilo la biashara, ghafla akapigwa na mshangao baada ya kuona jeneza likiwa mbele ya mlango wa mgahawa wake.
Umati wa watu uliofika kushuhudia tukio hilo.
“Nashindwa kujua nini maana ya tukio hili sababu hivi
karibuni nilikuta barua imebandikwa ukutani ikinitaka nihame kutoka eneo
hili, vinginevyo nitaona nitakachofanyiwa. Leo nimekuta jeneza
mlangoni,” alisema Ester na kuongeza;
“Tukio hili nalihusisha na imani za kishirikina lakini kubwa
linachangiwa na wivu wa kibiashara.Tangu lizaliwe sijawahi kuona jambo
kama hili. Hapa sijawahi kugombana na mtu yeyote nashangaa kufanyiwa
kitendo cha namna hii katika eneo la biashara
yangu.”
Difenda ya polisi ikiondoka eneo la tukio na jeneza hilo kuelekea makaburini.
--
--
Mwenyekiti wa mtaa huo, Anthony Deus alisema kitendo cha kufukua mwili wa marehemu tena mtoto mchanga, si cha
kibinadamu na ni tukio la kusikitisha katika jamii, hivyo watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.
Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza,
ACP Christopher Fuime, alikiri kuwapo kwa tukio hilo na kusema hakuna mtu aliyekamatwa akihusishwa nalo.
Mwili wa mtoto ukizikwa mara ya pili.
--
--
“Tunaendelea na uchunguzi lakini hadi sasa hakuna
aliyekamatwa akihusishwa na tukio hili la kusikitisha… wananchi
wameuzika upya mwili wa mtoto huyo,” alisema
Comments
Post a Comment