MCHEZAJI
ghali zaidi Duniani, Gareth Bale hajagusa hata nyasi za Bernabeu baada
ya kuvunja rekodi ya Dunia ya usajili kwa dau la pauni milioni 86,
lakini shida zimeshaanza katika chumba cha kubadilishia nguo katika
klabu ya Real Madrid.
Thamani
ya Mesut Ozil kwa wachezaji wenzake wa Real Madrid ilionekana jumatano
jana wakati wachezaji walikuwa wanapiga kelele za kumkubali huku
wakisema haina shida Bale atarithi mikoba yake.
Kwa
upande wa nyota wa Ureno na klabu hiyo, Cristiano Ronaldo amenyong`onyea
baada ya kumpoteza Ozil, wakati huo huo nao Alvaro Arbeloa, Isco na
hata nyota wa wapinzani wao, FC Barcelona, Cesc Fabregas wamekerwa na
kitendo cha Mjerumani huyo mwenye kipaji cha juu kuondoka ligi ya
Hispania.





Comments
Post a Comment