MNYAMA KUJIPIMA UBAVU NA KMKM KESHO TAIFA….MCHAKATO WA KATIBA WASHIKA KASI KIDIJITALI ZAIDI, MASHABIKI KUTUMA MAONI KWA E-MAIL!!
WEKUNDU
wa Msimbazi, Simba wanatarajia kushuka dimbani katika mchezo wa
kirafiki utakaofanyika kesho Ijumaa, Septemba 6 mwaka huu dhidi ya
mabingwa wa soka wa Ligi Kuu ya visiwani Zanzibar, KMKM, Uwanja wa Taifa
mjini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa iliotolewa na Afisa habari wa klabu ya Simba, Ezekiel
Kamwaga inafafanua kuwa lengo kuu la mechi hiyo ni mazoezi ya klabu hiyo
kujiandaa na mchezo wake wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mtibwa
Sugar, Septemba 14 mwaka huu uwanja wa Taifa.
“Kikosi
kamili cha KMKM kimewasili mjini Dar es Salaam tayari na leo saa tano
na nusu kamili nahodha wake, Abdi Kassim Babi na kocha mkuu wa timu hiyo
wanatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari katika mgahawa wa City
Lounge katikati ya jiji”. Alisema Kamwaga.
Kamwaga
ameongeza kuwa Simba inaendelea na mazoezi yake jijini Dar es salaam na
wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa ajili ya mechi
hiyo.
Afisa
habari huyo alifafanua kuwa mechi hiyo itaanza majira ya saa 11 jioni
ili kuwezesha watu wengi kwenda uwanjani kutazama mechi hiyo
ikizingatiwa kuwa Ijumaa ni siku ya kazi.
Mechi
hiyo inakuja muda mfupi baada ya kufanyika mechi maalumu septemba 2
mwaka huu ya kuwatambulisha nyota wake wapya, Henry Joseph, Gilbert Kaze
na Amisi Tambwe dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar ambapo Simba waliibuka na
ushindi wa mabao 4-3 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wakati huo huo Kamwaga ameeleza kuwa: Kufuatia tangazo la Mwenyekiti wa
Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, kuhusu Mkutano wa Katiba uliopangwa
kufanyika Novemba mwaka huu, klabu imeanzisha rasmi mchakato wa kuwa na
Katiba Mpya itakayokwenda na wakati.
Kutokana na umuhimu wa mawazo ya Wana Simba ndani na nje ya nchi
kufahamika kupitia mchakato huu, klabu imeanzisha email maalumu iitwayo
maoniyakatibayasimba@gmail.com ambapo wana Simba na wapenzi wa soka kwa
ujumla wanatarajiwa kuwasilisha mawazo na michango yao kuhusu nini
kinapaswa kuingizwa katika Katiba mpya ya klabu.
Uongozi wa Simba unawaomba wapenzi na washabiki wa soka popote walipo
duniani kuchangia mawazo katika njia hii. Mawazo yatakayochangiwa kwenye
email hii yatatumika katika kutengeneza rasimu ya Katiba hiyo na rasimu
hiyo itapelekwa kwenye matawi yote ya klabu kwa ajili ya kujadiliwa na
wanachama.
Mawazo hayo ya wanachama yatasaidia katika kutengeneza Katiba ambayo
hatimaye itawasilishwa kwenye Mkutano wa Novemba kwa ajili ya mapitio na
kupitishwa.Wana Simba wanatakiwa kujitokeza katika mchakato huu kwa faida ya kujenga Simba ya kisasa na yenye tija na ufanisi
Comments
Post a Comment