BRAZIL WAWEKA BONGE LA REKODI…HAIJAWAHI KUTOKEA TANGU KOMBE LA DUNIA KUANZA 1930, YACHAPWA NYUMBANI 7-1 NA UJERUMANI
Na Baraka Mpenja
KWA
Muda mrefu wananchi wa Brazil waliandamana wakipinga nchi yao kuandaa
fainali za kombe la dunia kwasababu kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa.
Walikuwa
wakihuzunishwa na matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya kuandaa miundo
mbinu ya kombe la dunia, wakati maisha yao yakiwa katika hali mbaya.
Huduma mbovu za jamii, umasikini wao uliwahamasisha kuandamana na kuleta sintofahamu ya kisiasa.
Brazil
walienda kwa kujivuta na mnamo juni 12 mwaka huu wakasahau shida zote
na kushuhudia timu yao ya Taifa ikicheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya
Croatia.
Walipata ushindi wa mabao 3-1 na kufurahia matokeo hayo.
Faraja
pekee kwa wananchi maskini wa Brazil ilikuwa ni kuona timu yao inafanya
vizuri na kubeba kombe. Walikuwa wanafurika uwanjani, kwenye kumbi za
kuoneshea mpira, lengo ni kutaka kuona timu yao inafanya nini.
Brazil ambayo unaweza kusema ni mbovu kuliko Brazil zote zilizopita, ilijikongoja hatua ya makundi na kuingia hatua ya 16.
Baada
ya hapo walipigiwa mbungi kubwa na Colombia, lakini walifanikiwa
kusonga mbele kwa mikwaju ya penati na kutinga nusu fainali.
Kwa bahati mbaya wakiwa na ubovu wao, waliingia mikononi mwa `watu katili`, Ujerumani.
Kabla
ya mechi, kocha Luiz Felipe Scorali alijigamba kuifunga Ujerumani na
katika mkutano wa jana na waandishi wa habari alithubutu kuuzungumzia
mchezo wa fainali, tena dhidi ya Argentina.
Kwa bahati mbaya hakufirikiria kama anaenda kukutana na Ujerumani yenye bunduki zote.
Mlinda mlango, Julio Cesar hakuwa na ujanja wa kuzuia mpira uliopigwa na Muller, huku David Luiz akishangaa .
Brazil ambayo unaweza kusema ni mbovu kuliko Brazil zote zilizopita, ilijikongoja hatua ya makundi na kuingia hatua ya 16.
Baada
ya hapo walipigiwa mbungi kubwa na Colombia, lakini walifanikiwa
kusonga mbele kwa mikwaju ya penati na kutinga nusu fainali.
Kwa bahati mbaya wakiwa na ubovu wao, waliingia mikononi mwa `watu katili`, Ujerumani.
Comments
Post a Comment