HAYA YA BRAZIL KUPIGWA 7-1 NI MAJANGA, KWA SIMBA SC MUDA WA KUPANGA MAJESHI UMEFIKA, FANYENI HAYA…….
LUIZ Felipe Scolari amekubali kubeba lawama zote kutokana na fedheha waliyoipata Brazil kutoka kwa `watu katili` Ujerumani.
Haikutegemewa na wengi kama Brazil
wangeingia katika rekodi mbaya ya kombe la dunia kwa kufungwa mabao 7-1
na Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia jana
usiku.
Brazil waliojiamini, waliingia kwa
kasi, lakini bao la mapema la Thomas Muller liliwatoa upepo ghafla ya
kufungisha mabao mengi zaidi.
Bora Neymar hakuwepo katika mchezo
huo. Huyu ni mchezaji mwenye kiwango cha juu kama alivyo kwa Lionel
Messi na Cristiano Ronaldo.
Kama angekuwepo uwanjani, halafu Brazil ikafungwa mabao kama ya jana, basi ingemharibu zaidi katika maisha yake ya soka.
Tatizo kubwa la Brazil lilikuwa
kwenye safu ya ulinzi iliyoongozwa na nahodha David Luiz, Maicon,
Marcelo na Dante. Hawa walikuwa tatizo jana, walikaba vibaya, utulivu
ulikuwa `F`. Hata Neymar angekuwepo, kwa aina ya uchezaji wake, bado
safari ya Brazil ingefika mwisho kwasababu asingekuwa na jinsi ya
kuwaokoa.
Mambo ya `wedi kapu` haya, si mchezo: David Luiz alishindwa kuzuia machozi baada ya `mbungi` kumalizika.
Pole sana Scolari, pole sana
Neymar, Pole sana Thiago Silva, pole sana wananchi wa Brazil, pole sana
mashabiki wa Brazil duniani kote. Huo ndio mpira wa miguu, Rekodi yenu
itazungumzwa zaidi ya miaka 50 ijayo.
Hongereni Ujerumani kwa ushindi
mnono. Hongereni kwa Miroslav Klose kuvunja rekodi ya gwiji wa Brazil,
Ronaldo. Mabao 16 na kuwa mfalme wa mabao wa kombe la dunia ni heshima
kubwa.
Comments
Post a Comment