Swali: Kuna wasanii wengi kutoka Tanga lakini wewe umetoka mapema. Unazungumziaje msoto uliopitia hadi ukatusua kimuziki?
Roma Mkatoliki (kulia) akifunguka wakati akihojiwa na prizenta wa Global TV Online, Pamela Daffa 'The Mic Queen'
Roma: Ni kweli Tanga kuna wasanii wengi kama ilivyo Kigoma. Tuna-fight sana na Kigoma. Kuhusu msoto siyo kwa wasanii wa Tanga tu
hata sehemu nyingine kuna msoto. Kwa Roma ilikuwa rahisi kwa sababu
alisoma gemu akagundua kuna vitu fulani havijaguswa ndipo nikapita
hukohuko.
Swali: Roma ni staa mkubwa wa Hip Hop Bongo. Je, ni kichwa kipi kingine unakikubali?
Roma: Wapo watatu. Wa kwanza ni Roma, wa pili ni Roma na wa tatu ni Roma.
Swali: Kwa nini Roma?
Roma: Najikubali sana ndiyo maana najiona namba moja, mbili na tatu.
Swali: Wewe ni mmoja wa wana-hip hop wasomi. Umemaliza UDSM Mlimani. Kwa nini ukaegemea kwenye muziki badala ya kuajiriwa?
Roma: Siyo kwamba sijawahi kuajiriwa. Kwanza hata fedha ya kwenda
studio nilidunduliza mshahara. Ni kweli nimesoma Kompyuta Sayansi pale
Mlimani. Sijaajiriwa. Muziki nao ni ajira.
Swali: Kuna hii system ya wasanii kutoa singo na kuachana na albam. Kwa mtazamo wako inalipa zaidi ya albam?
Roma: Miaka ya 90 kuja 2000, wasanii walitumia mtindo wa albam. Akina
Mr Nice, Profesa J na hata Sugu waliwahi kuingia mkataba na wakalipwa
fedha nyingi za albam.
Baadaye situation ilibadilika. Kukawa na
malalamiko mengi kwamba msambazaji ambaye alikuwa ni mmoja tu Mamu
alikuwa anawanyonya.
Ndipo wasanii wakaamua kutoa singo, video na kufanya shoo. Hapa ndipo
akina Adam Juma walipokuwa maarufu. Ndicho kipindi ambacho Roma
amekikuta. Tunatoa albam, tunafanya shoo, tunatoa mix tapes watu
wanasikiliza mtaani kwenye bodaboda. Labda kizazi kingine kitakachokuja
huko mbele kinaweza kuwa na system nyingine labda matangazo, kuuza
muziki mitandaoni kama itunes na makampuni kuamua kutumia wasanii kwenye
shughuli mbalimbali lakini kwa sasa ni mwendo wa singo na shoo ambazo
kwa sasa tuache uongo zinalipa.
Swali: Kwa nini unapenda kwenda Tanga?
Roma: Mimi na familia yangu tunaishi Dar, napenda kwenda Tanga ndipo wazazi wangu walipo, nimezaliwa Tongwe.
Swali: Roma unatumia mtindo wa kukosoa watu kwa maneno ya ukali. Je, unakutana na vitisho vyovyote?
Roma: Ili kufikisha ujumbe au kukemea jambo lazima useme kwa ukali.
Ninachokisema ndicho kilicho kwenye mawazo ya watu ndiyo maana kwenye
shoo huwa nakusanya kijiji. Sijakutana na vitisho lakini kuna baadhi ya
media namaanisha redio hawapigi nyimbo za aina fulani kwa sababu ama
maadili au masilahi yao.
Hilo nina uzoefu nalo nimeshakutana nalo sana ndiyo maana nikabuni
system mpya ya bodaboda. Ngoma yangu isipopigwa redioni then itapigwa
kwenye bodaboda na nikikutana nao kwenye shoo tunaenda sawa.
Swali: Roma huwa unawaimbisha watu na wanakuelewa, je, unatumia kitu gani kupata ule mzuka?
Roma: Ile inaitwa vibe, ukiwaambia twende hivi wanaenda. Hii inategemea
vitu vingi kama sound, malipo mazuri, dj mkali na steji yenyewe. Kuhusu
kilevi mimi situmii chochote ishu ni kucheza na raia tu.
Swali: Kwa nini wasanii wa Hip Hop ni wachache?
Roma: Ni wengi
sana. Hata underground wapo wengi. Mimi niliangalia nikaona nifanye kitu
tofauti so ni namna tu utakavyoweza kupenya.
Swali: Uhusiano wako na Weusi ukoje? Je, kuna mpango wowote wa kolabo?
Roma: Uhusiano upo fresh. Joh Makini, Nikki tupo poa sana. Sina bifu na
Weusi. Hakuna matatizo yoyote. Kwani kuna tatizo? Mimi sina matatizo.
Kuhusu kolabo kuna watu wengi sijafanya nao, yupo Profesa J, Fid Q,
marehemu Ngwea nilitamani kufanya naye. So siyo Weusi tu wapo wengi.
Weusi wanaiwakilisha vyema Arusha.
Swali: Ni singo gani za kwako ambazo zimefanya poa kwa kipindi chote cha muziki wako?
Roma: Almost singo zote kuanzia Kidole cha Mwisho, Tanzania, Ngoma za Ugenini, Mr President, Mathematics, 2030 hadi KKK.
Swali: Roma wewe ni Muislam au Mkristo kwa sababu kumekuwa na
mkanganyiko? Roma: Naitwa Ibrahim Musa. Ni Mkristo wa Kanisa Katoliki.
Ndiyo maana ukisikiliza mashairi yangu utakutana na mistari ya Biblia
ambayo nilijifunza tangu mafundisho.
Swali: Una mpango wa kujishughulisha na siasa? Je, una mke na mtoto?
Roma: Naliamini sana jukwaa nililopo na naliheshimu. Sehemu ambayo nipo
ni sahihi kuliko sehemu yoyote. Sina mpango wa kugombea. Kuhusu mke,
yupo na nina mtoto mmoja.
Comments
Post a Comment