Katibu Mtendaji wa Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa tatu kushoto) akipata
maelezo kuhusu Mradi wa Chuma Liganga kutoka kwa Nie Zhiyan (kulia),
ambae ni Makamu Ofisa Muendeshaji Mkuu wa Tanzania China International
Mineral Resources Ltd (TCIMRL). Hili ni eneo ambalo kiwanda cha chuma
chenye uwezo wa kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka kitajengwa. Kutoka
kushoto, wengine ni Bw. Ramson Mwilangali, Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda
Mama – NDC , Bw. Erasmus Masumbuko, Mchumi – Tume ya Mipango, Bw. Maduka
Kessy, Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, anaeshughulikia Sekta za
Uzalishaji, Bw. Israel Mkojera Makamu Meneja Utawala – TCIMRL, Bi.
Florence Mwanry Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango anaeshughulika na
Huduma za Jamii na Idadi ya Watu na Bw. Mlingi E. Mkucha, Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa NDC.
Mlima wenye madini ya chuma, ambapo shughuli ya uchimbaji wa chuma unategemea kuanza
kutekelezwa. Uzalishaji wa chuma unatarajiwa kuanza mwaka 2016.
Viongozi na Maofisa kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiwa katika eneo ambalo uchimbaji wa
chuma utatekelezwa. Pamoja nao ni Viongozi kutoka National Development
Corporation (NDC) na Tanzania China International Mineral Resources Ltd.
Nyuma ni kilima ambacho kimejaa utajiri wa mawe yenye madini ya chuma
ambapo jiwe linakadiriwa kuwa na chuma kwa 52%.
Viongozi na maofisa kutoka Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango (ORTM), National Development Corporation (NDC)
na Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMR) wakiwa
pamoja na viongozi wa Kijiji cha Mundindi ambapo ni eneo ambalo Mradi wa
Uchimbaji wa Chuma utatekelezwa. Viongozi hawa pamoja na wanakijiji
wameonyesha ushirikiano mzuri na mwekezaji katika kufanikisha
utekelezaji wa mradi.
Timu kutoka Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa wataalam wa kampuni ya Tanzania
China International Mineral Resources Ltd kuhusu Iron Ore Samples
zilizopatikana wakati wa utafiti kuhusu wingi na ubora wa chuma
kitakachopatikana katika eneo la Liganga.
Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango Dkt. Philip Mpango (aliyesimama) akiongea na Viongozi
wa Kijiji cha Mundindi pamoja na viongozi na wataalam wa kampuni ya
Tanzania China International Mineral Resorces Ltd
Comments
Post a Comment