Skip to main content

WAZIRI MKUU: MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA YANAENDELEA

1(5)WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu yanaendelea japo kwa kiasi kikubwa hatma yake inategemea kukamilika kwa mchakato wa Katiba mpya.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Juni 30, 2014) wakati akizungumza na Mameya wa Majiji, Manispaa na Wenyeviti wa Halmashauri za Miji na Wilaya Tanzania katika kikao cha siku moja kilichofanyika kwenye ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga.
Waziri Mkuu yuko Tanga kwa ajili ya sherehe za Serikali za Mitaa ambayo kilele chake kitafanyika kesho Julai mosi kwenye uwanja wa Tangamano jijini hapa. Ameamua kukutana na viongozi hao ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya kukutana nao aliyoitoa Mei 14, 2014 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa ALAT.
“Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bado ni kitendawili kwa sababu kwa kiasi kikubwa inategemea sana kukamilika kwa Mchakato wa Bunge la Katiba,” alisema na kuongeza:
“Kama Wizara tunaendelea na maandalizi tukiamini uchaguzi upo, kama hiyo fursa isipotokea bado tutakuwa tumekamilisha maandalizi kwa upande wetu.Tunaendelea kuandaa kanuni kwa kushirikisha wadau wote,” alisema.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kusisitiza suala la ukusanyaji mapato na udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali. Kuhusu mapato, Waziri Mkuu alisema katika mwaka wa fedha wa unaoisha sasa, hali ya ukusanyaji mapato haikuwa nzuri.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu alisema amewaandikia barua Wakuu wa Mikoa akiwataka waweke utaratibu wa kutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu juu ya makusanyo ya kila Halmashauri zilizo kwenye mikoa yao.
“Katika taarifa hizi itabidi kila Halmashauri ieleze ilipanga kukusanya kiasi gani, je imefikia lengo na kama sivyo ni kwa nini. Nia yetu ni kutrack down makusanyo na kuona yamekwama wapi na yamekwamishwa na nini,” alisema.
Kuhusu udhibiti wa matumizi, Waziri Mkuu aliwataka Mameya na Wenyeviti hao kuendelea kuwabana wahusika ili kudhibiti matumizi yasiyofaa. “Lazima muendelee kuwabana na kuwasimamia wakurugenzi na wataalaam wa kwenye Halmashauri zenu. Fanyeni kazi kwa ufanisi, msiwachekee wale wanaoharibu,” aliongeza.
“Ili muweze kuwabana vizuri, ni lazima mdai kupatiwa taarifa za fedha kutoka kwa Mkaguzi wa Ndani (Internal Auditor)… kuna baadhi ya watendaji wanadai kuwa hizi taarifa ni siri wakati siyo siri,” alisema.
Aliwaeleza washiriki wa kikao hicho kwamba taarifa hizo ni muhimu kwao kuzipata na zitawasaidia kuonyesha mapungufu yoyote kama yapo.
Aliwataka kila mmoja wao kwa nafasi zao za Meya na Mwenyekiti wahakikishe wanalenga kupandisha pato la wananchi wanaowaongoza.

Comments

Popular posts from this blog

VIDEO YA NGONO YA WANAOSADIKIKA KUWA NI WANAFUNZI WA IFM YAVUJA

Watu wawili wanaosadikika ni wanachuo wa IFM wajirecord video wakifanya ngono ndani ya........... chumba ambacho kinaonesha kama ni cha hosteli, fungua na uone upuuzi uliofanyika humu ndani…. KUANGALIA VIDEO HII LAZIMA UWE NA UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18+ KUANGALI BOFYA HAPA

Huyu Mzee Ndio Aliyetia Aibu Kwenye Bar Hii yenye Makahaba wanaocheza Nusu Uchi

 vijimambo kwenye bar zetu  

HUYU HAPA NDIYE MCHUNGAJI ADAI KUWAUA KANUMBA NA SHARO MILIONEA, AELEZEA JINSI ALIVYOFANYA....WAUMINI WAPIGWA NA BUTWAA..

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘ The Great’ . Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda. Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda. VIFO MILIONI 605  Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini. Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao. WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kun...