Serikali ya Syria bado haikusema kitu kuhusu taarifa
kutoka wakuu wa Marekani kwamba ndege za Israel zimefanya mashambulio
katika ardhi ya Syria, ambako inaarifiwa ghala ya silaha imeshambuliwa.
Wakuu wanasema makombora yalifyatuliwa kutoka ndege za Israel ambazo ziliruka kwenye anga ya Libnan, nchi ya jirani.
Huku nyuma kuna taarifa za mauaji zaidi katika miji ya pwani ya Syria kukiwa na tuhuma kuwa raia wengi wamechinjwa na wanajeshi wa serikali na wanamgambo.
Wanaharakati wanaripoti kuwa mauaji ya pili yamefuatia yale ya kwanza katika eneo hilo-hilo la mwambao kaskazini-magharibi mwa Syria.
Wanasema mauaji ya kwanza yalifanywa kwenye kijiji cha al-Beida cha Wasunni, ambacho kilivamiwa na wanajeshi wa serikali siku ya Alkhamisi.
Wanaharakati wamewataja watu 50 ambao wanasema walichinjwa kati yao wakiwemo wanawake na watoto.
Sasa wanaeleza kisa kama hicho kutokea katika mtaa wa Ras an-Naba wa mji wa pwani wa Banias ulio jirani na al-Beida.
Wameonesha picha kwenye internet kama ushahidi, lakini hakuna njia ya kuthibitisha ukweli wa picha hizo.
Picha zinaonesha maiti za wanawake na watoto zimelala ndani ya nyumbao zao, miili mengine imekeketwa na mengine imechomwa.
Mamia ya familia zimekimbia Banias kuelekea kusini kwenye mji wa Tartous, lakini wanaharakati wanasema wakimbizi hao wamezuwiliwa kupata hifadhi katika mji huo.

Comments
Post a Comment